Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira yaendelea na Ziara yake ya kutembelea Viwanda katika Mkoa wa Pwani ili kusikiliza changamoto mbalimbali za Viwanda, Kamati leo tarehe 16 Ogasti, 2018 imetembelea kiwanda cha Bakhresa Food Products Ltd (BFPL) kiwanda kinachosindika matunda na vinywaji baridi, maji ya kunywa na juisi inayotokana na matunda yanayozalishwa nchini.

Kiwanda kina uwezo wa kusindika matunda tani 330 kwa siku kwa matunda yanayotoka katika mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga, Iringa, Shinyanga na Tabora.Katika Ziara hiyo kamati ya Bunge imejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho na kupongeza uongozi wa kiwanda kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika ambao umesaidia nchi kupata kodi pia ajira kwa watanzania.

Aidha uongozi wa Kiwanda umeeleza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo zikiwemo wingi wa taasisi za udhibiti ubora, kodi kubwa inayotozwa wakati wa uingizaji wa makasha maalumu ya kuhifandhia matunda, Stika za kodi za kieletronic (ETS), na Vikwazo visivyokuwa vya kikodi kwa bidhaa za Azam Mango na Azam energy kuuzwa kwa wateja nchini Kenya.

Kamati imehitimisha Ziara yake kwa kutembelea kiwanda cha Lodhia kilichopo Mkuranga kinachotengeza nondo, mabomba na matenki ya kuhifadhia maji.Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akiwa na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya biashara katika kiwanda cha bakhressa. 
  
 Picha ya Pamoja.
Wabunge wakitembele kiwanda cha cocakola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...