Kamishna wa Huduma za Parole,Viwanda, Huduma za jamii na Programu za Urekebishaji Af. Augustine Mboje  Sangalali(suruali nyeupe) akisalimiana na Mkuu wa Kilimo,Mifugo na Utunzaji wa Mazingira, Kamishna Msaidizi  Mwandamizi wa Magereza Mlasani Deodath Kimaro, alipotembelea Banda la Magereza katika maonesho ya Nane nane yanayofanyika Kitaifa Nyakabindi,Wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.
 Sajini Caroline Mtolera wa Jeshi la Magereza akimuelezea Af. Kamishna Mboje namna ya kutunza mazingira kwa kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya taka ngumu.

 Kamishna Mboje akipata maelezo ya shamba darasa toka kwa Mrakibu Msaidizi wa Magereza Nimwindaeli Mzirai alipotembelea banda la Magereza kwenye Nane nane inayofanyika Nyakabindi,Bariadi Mkoani Simiyu.
 Sajini Mateso Alex Linze wa Magereza akimuelezea Kamishna Mboje jinsi ya utunzaji Samaki kwa njia ya kisasa huku banda la kuku likiwa juu ya bwawa la samaki hao.

 Sajini Mahimbo Dafa akimuelezea Kamishna Mboje njia bora na sahihi ya Uhamilishaji wa mbegu za ng’ombe ili kupata mifugo ya kisasa na yenye afya.
Wada Mwinyi  Onanda wa Magereza akimunesha na kumuelezea  Kamishna Af. Mboje mazao mbalimbali yanayolimwa na Magereza mbalimbali kama njia ya urekebishaji wa wafungwa. Picha na Jeshi la Magereza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...