Mkuu wa wilaya Uvinza Mwanamvua Mrindoko (wa nane kushoto) kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Kigoma Emanuel Maganga (hayupo pichani) akipokea kwa pamoja na wadau na watumishi mbalimbali msaada kutoka kwa Mkuu wa masoko na mawasiliano wa Benki ya Exim Stanley Kafu (wa nne kulia) wa vitanda na magodogoro 50 yaliyotolewa na Benki ya Exim kusaidia upungufu wa vitanda kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni. Hospitali ya Maweni mkoani Kigoma ni hospitali ya kumi na mbili kupata msaada wa vitanda na magodoro kutoka Benki ya Exim Tanzania.
Baadhi ya watumishi na wadau mbalimbali waliohudhuria tukio la Benk ya Exim kukabidhi vitanda na magodoro kwa hospitali ya mkoa Kigoma Maweni. 
Mkuu wa wilaya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko (aliyesimama katikati)  akizungumza muda mfupi kabla hajapokea kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Kigoma, Emanuel Maganga (hayupo pichani) msaada wa vitanda na magodogoro 50 yaliyotolewa na Benki ya Exim kusaidia upungufu wa vitanda kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni. Wa pili kulia ni  Mkuu wa masoko na mawasiliano wa Benki ya Exim Stanley Kafu (na kushoto) ni Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Shaban Mchata. 


BENKI ya Exim Tanzania leo katika kukamilisha kampeni yake ya miaka 20 ya kujali jamii imekabidhi vitanda na magodoro 50 kwa Hospitali ya Maweni mkoani Kigoma. Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo imewekeza shilling milioni 200 katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake.
Hospitali na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa, benki ya Exim Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa imeanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika wodi za wazazi kwenye hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali k
atika mikoa mbali mbali nchini kama sehemu ya kampeni yake ya mwaka yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.
Hospitali ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni ni hospital ya kumi na mbili kupokea mchango huu, baada ya hospital ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro mwezi Juni, hospitali ya serikali ya Sekou Toure ya mkoani Mwanza mwezi Mai, hospitali ya rufaa ya Morogoro mwezi Aprili, hospitali ya rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam mwezi Machi, hospitali  ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mwezi Febuari, hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya mwezi Januari, hospitali ya Mount Meru, Arusha mwezi Desemba, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka jana. 
Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo katika wodi ya wazazi na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Uvinza, Kigoma Mwanamvua Mrindoko, Mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu na Mkurugenzi wa hospital ya Maweni mkoani Kigoma Dk. Osimund Dyegura.
Mkurugenzi wa hospital ya Maweni mkoani Kigoma, Dk. Osimund Dyegura alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya kwa nchini. Aliongezea kwa kusema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 50 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii.”
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano, Mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu alisema, “Benki imetambua umuhimu wa jumuiya zinazozunguka eneo la biashara yetu na ndio maana shughuli za kijamii ni muhimu sana kwa Benki ya Exim. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa katika kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu. 
Ni kwa hili Benki iliamua kusherehekea miaka 20 kwa kusaidia jamii kwa njia ya kampeni inayoitwa, “miaka 20 ya kujali jamii” kuonyesha jinsi tunavyowashukuru. Japokuwa mradi huu umefikiwa ukingoni Benki ya Exim itaendelea kutoa misaada katika sekta ya afya kwenye hospital mbali mbali nchini.”
Benki ya Exim ilitambuliwa kama benki bora kwa huduma ya wateja binafsi mwaka 2017 inasheherekea miaka 20 ya mafanikio, ukuaji na kuwa kiongozi katika kuingia katika masoko mapya barani Afrika. Benki ya Exim ilianzishwa mwaka 1997 na imetanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu katika nchi za Comorro (2007), Djibouti (2010) na Uganda (2016).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...