Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuonya mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kwa kushindwa kuwasiliana na mdhamini wake na kutoa sababu za msingi mahakamani.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa onyo hilo leo Agosti 6,2018 wakati kesi ya kufanya maandamano yasiyo halali inayowakabili viongozi 9 wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezi ya awali.

Kabla ya kutolewa onyo hilo, wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameeleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa PH lakini mawakili wa utetezi hawakufika mahakamani.Wakikli Hekima Masipo alidai mahakamani hapo kuwa Wakili wa washtakiwa Peter Kibatala yupo Mahakama kuu huku Jeremiah Mtobesya akiwa katika kesi nyingine Mtwara.

Hata hivyo, mahakama ilimtaka mshtakiwa wa 5, Esther Matiko ambaye hakufika mahakamani hapo tarehe iliyopita na shahidi wake akaeleza kuwa alipatwa n dharura, basi aelezee hiyo dharula yake.Matiko amedai kuwa alipigiwa simu ya dharura kwenda shuleni anaposoma mwanaye Agosti 1, 2018 na akaondoka saa 4 usiku. Ambapo baada ya kufika shule aliambiwa mtoto wake ni mgonjwa na alipompeleka hospital alikutwa na Tetekuwanga na akaambiwa apumzike kwa siku 4.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri alimuhoji Matiko kuwa mbona mdhamini wake alishindwa kuieleza mahakama kwamba amekwenda Kenya kufanya nini."Nakupa warning mara nyingine uwe muwazi, hii iwe mara ya mwisho, siku nyingine unapaswa kumueleza mdhamini wako ni dharura gani imekupata," Hakimu Mashauri.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 13.2018 kwa ajili ya washtakiwa kuja kusomewa PH.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakiwa kwenye moja ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kusikiliza kesi  yao


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...