Na Grace Gwamagobe,  Songwe

Ongezeko la hali ya udumavu Mkoani Songwe inachagizwa na kuwa ni asilimia 25 pekee ya akina mama wote wanaojifungua ndio huwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Kheri Kagya ameeleza kuwa udumavu mkoani hapa ni asilimia 37.7 ikiwa na maana kuwa kati ya watu 100, 37 wanatatizo la udumavu kiwango ambacho ni kikubwa licha ya Mkoa Songwe kuwa na Vyakula vya kutosha.

“Moja ya sababu kubwa ya ongezeko la udumavu Mkoani kwetu ni kutokana na akina mama wanaojifungua kutowanyonyesha watoto wao maziwa pekee kwa kipindi cha miezi sita, hali hii huwafanya watoto kukosa virutubisho muhimu katika hatua za awali za ukuaji”, amesema Dkt Kagya.

Ameongeza kuwa maziwa ya mama hujenga afya imara kwa watoto hivyo akina mama wanaojifungua wazingatie ushauri wa wataalamu wa afya wa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee kwa miezi sita, na kisha kuendelea kunyonyesha na vyakula vingine mbadala mpaka mtoto afikishe umri wa miaka miwili.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Kheri Kagya akitoa zawadi kwa akina mama wa mfano walioweza kunyonyesha watoto wao maziwa pekee kwa muda wa miezi sita wakati wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Akina mama wa mfano walioweza kunyonyesha watoto wao maziwa pekee kwa muda wa miezi sita wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na afya ya mama na mtoto mkoa wa Songwe.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...