Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko Lusubilo, Kigoma Bw. Joeli Mwakibibi akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura Jumamosi Agosti 11, 2018 wakati wa mafunzo ya Kusimamia uchaguzi  mdogo wa Ubunge utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.
 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko Lusubilo, Kigoma Bw. Joeli Mwakibibi akiwaapisha Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura Jumamosi Agosti 11, 2018 ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kufuata sheria wakati wa mafunzo ya Kusimamia uchaguzi  mdogo wa Ubunge utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Uchaguzi katika jimbo la Buyungu (hawapo pichani), wilayani Kakonko wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kusimamia Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo Jumamosi Agosti 11, 2018.
 Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kiziguzigu Bi. Jesca Masawe akifafanua jambo kwa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura wakati wa mafunzo ya kusimamia uchaguzi mdogo katika jimbo la Buyungu leo.
 Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ya Kakonko  Bi. Martina Ulungi akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kufunga lakiri (seal) za usalama kwenye maboksi ya kura wakati wa mafunzo kwa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura leo wilayani Kakonko.
 Mafunzo kwa vitendo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo jimbo la Buyungu yakiendelea leo katika jimbo la Buyungu.
Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya kupigia Kura wakifanya mazoezi kwa vitendo ya kufunga vituturi vya kupigia Kura vitakavyowekwa kwenye vituo vya kupigia Kura wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kusimamia uchaguzi mdogo leo wilayani Kakonko.
PICHA KWA HISANI YA NEC/BUYUNGU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...