Na Frankius Cleophace Tarime.

Mabinti 40 ambao wako nje ya mfumo rasmi wa shule kutoka kata tano wilayani Tarime Mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya ujasiramali kwa lengo la kuongeza mbinu, sifa na dhana bora katika kufanya shughuli zao za baishara ili kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kuondokana na utegemezi.

Mabinti hao baadhi yao hawakubahatika kwenda shule na wengine wao wamekatisha masomo kwa kupatiwa ujauzito wakiwa shuleni ,wengine kuolewa katika umri mdogo kutokana na mila na desturi ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike, huku wengine wakiwa kwenye ndoa japo wameolewa katika umri mdogo, na baadhi wameshindwa kumudu ndoa hizo na kuachika hapa kilio chao kikubwa ni kuomba Serikali kwa kushirikiana na shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime kuwapatia Mitaji pamoja na Malighafi baada ya kupatiwa ujuzi.

Magreth Kichele kutoka kata ya Komaswa ameiomba serikali kwa kushirikiana na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto kuwapatia malighafi pamoja na vifaa ili waweze kujitegemea na kuendeleza biashara zao huku wakionyesha tofauti baada ya kupatiwa elimu hiyo ya siku tatu na kuhaidi kwenda kufanyia kazi elimu hiyo waliyopewa.

“Sisi tunaishi vijijini tunamaisha magumu sasa kama tumepatiwa elimu changamoto kubwa ni mitaji wengine wanavyereani hawana pesa za kununu malighafi hivyo sasa shirikal na serikali wakishirikiana wakatusaidia tutashukuru sana” alisema Magreth.

Kambibi Kamugisha kutoka shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime akitoa ufafanuzi jinsi mafunzo hayo yalivyotolewa kupitia Shirikal hilo kwa kushirikiana na Shirika la Plan Internation Tanzania chini ya Ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Sweden (Sida) pamoja na Shirika la Umoja wa Ulaya.
Washiriki wa Mafunzo hayo ambao ni mabinti 40 kutoka kata tano Halmashauri ya Tarime Vijijini wakiendelea kupatiwa elimu ya ujasiraimali.

Picha ya pamojana washiriki wa mafunzo hayo baada ya kupatiwa elimu ya ujasiriamali.Kambibi Kamugisha kutoka shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime akitoa ufafanuzi wa jambo katika Mafunzo hayo ya siku tatu katika ukumbi wa MCN Mjini Tarime Mkoani Mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...