Na Genofeva Matemu na Salome Majaliwa 

17/08/2018 Jumla ya wagonjwa 22 wenye matatizo ya moyo yatokanayo na mfumo wa umeme wa moyo usiofanya kazi sawasawa wamefanyiwa upasuaji mdogo na kuwekewa vifaa maalum vitakavyousaidia moyo kufanya kazi vizuri.

Matibabu hayo yamefanyika katika kambi maalum ya siku saba iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mgonjwa kufanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Magonjwa ya moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge alisema kambi hiyo inafanywa na madaktari wa Taasisi ya Moyo kwa kushirikiana na wenzao wa nchini Marekani kutoka Shirika la Madaktari Afrika.

Dkt. Kisenge alisema kambi hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo ambao mapigo yao yako chini kwa asilimia hamsini kwa dakika kwa kuwawekea kifaa maalum akinachosaidia mapigo ya moyo kuongezeka (Pacemaker).

“Kazi ya kifaa hiki maalum cha mfumo wa umeme wa moyo ni kuwasaidia wagonjwa wasipoteze maisha ghafla, kwani mara nyingi wagonjwa wenye matatizo ya mapigo ya moyo ambayo yako chini hufa vifo vya ghafla”, alisema Dkt. Kisenge.


Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakiangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo wa mgonjwa unavyofanya kazi kabla ya kumwekea kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Implantable cardioverter defibrillator – ICD) katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo. 
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakiandaa vifaa vitakavyotumika katika upasuaji mdogo wa kumuwekea mgonjwa kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Implantable cardioverter defibrillator – ICD) katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...