Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema umefika sasa kwa kwa Wizara na Taasisi zinazohusika na Sekta ya Elimu Nchini kumuandaa Mwanafunzi katika masomo ya Kilimo kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari ili atakapofikia uwezo wa kuingia chuo Kikuu awe tayari ameshaelewa nini Kilimo.
Alisema uingizwaji wa  Mitaala ya Kilimo ndani ya masomo ya kawaida maskulini itamuwezesha Wanafunzi kujitayarisha mapema katika muelekeo wa kujijengea uwezo wa ajira ya uhakika ndani ya Sekta ya Kilimo wakati amalizapo masomo yake ili aweze kujitegemea kupitia Sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri wakati akizungumza na vyombo mbali mbali vya Habari mara  baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia Maonyesho  mbali mbali ya Siku ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akivishwa Skafu na Vijana Chipukizi wa Morogoro mara alipoingia kwenye Unjwa wa Maonyesho wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akifurahia vifaa  zinazotengenezwa na mjasiriamali wa Mkoa wa Tanga
 Balozi Seif akinunua moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Wajasiri Amali kutoka Mkoani Tanga kwenye Maonyesho ya Nane Nane Morogoro.
 Moja ya Bwawa la kufugia Samaki la Chuo Kikuu cha sokoni Mkoani Morogoro ambalo Balozi Seif na Ujumbe wake walipata muda wa kulitembelea.
 Balozi Seif akiangalia ukulima wa mpunga uliooteshwa katika mfumo wa Taaluma ya kisasa kwenye Kitalu cha Kanisa la Anglican Dayosisi ya Morogoro kiliomo ndani ya Maonyesho ya Nane Nane.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...