Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili  Mjini Windhoek Namibia leo Agosti 15, 2018 kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), utakaofanyika tarehe 17 – 18 Agosti 2018.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia, Makamu wa Rais amepokelewa na  Waziri wa Elimu ya Juu , Mafunzo na Ubunifu wa Namibia Mhe. Dkt. Itah Kandjii – Murangi , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christin Hoebes na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Namibia.
Hii ni sehemu ya mikutano ya awali ya maandalizi ya mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia. 
Mikutano mingine ya awali ni pamoja na mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC uliofanyika tarehe 9 na 11 Agosti 2018 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa , Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2018 ambao utapitia na kujadili hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018. 
Mkutano huu utahusisha nchi tatu za SADC Organ TROIKA na wajumbe wake ambao ni Angola Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Zambia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Organ na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Mwenyekiti wa Organ aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi hiyo. 
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christine Hoebes alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli 
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga  alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli  
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christine Hoebes mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...