Na James Ndege – Dar es Salaam.
MAMLAKA ya Chakula na Dawa imekutana na wadau wapatao 50 kujadili udhibiti wa gesi tiba (medical gases) katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya TFDA tarehe 16 Agosti, 2018 kwa lengo la kulinda afya ya jamii. 

Mkutano huo umehusisha wadau bidhaa hiyo wakiwemo wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, hospitali,Wizara na taasisi za udhibiti za Serikali kutoka mikoa mbalimbali nchini. Katika mkutano huo, wadau walijadili na kuelezwa matakwa ya kisheria ya udhibiti wa bidhaa hiyo nyeti kwa afya ya binadamu. 

Mamlaka imeanza udhibiti wa bidhaa hiyo ambayo ipo katika kundi la bidhaa za Vifaa Tiba kuanzia mwezi Aprili 2018 ambapo katika kipindi cha mpito cha mwaka mmoja, wadau wametakiwa kuwasilisha TFDA orodha na taarifa ya bidhaa walizo nazo kwa utambuzi (notification) na kwamba waanze utaratibu wa usajili kwa kuwa kipindi cha utambuzi kitamalizika mwezi Aprili 2019 na baada ya hapo bidhaa ambazo hazijasajiliwa na TFDA hazitaruhusiwa kuingi katika soko. 

“TFDA inatarajia wadau wote kukidhi kwa hiyari matakwa ya kisheria ya udhibiti wa gesi tiba kwa muda uliopangwa ili kuepusha usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wale wataokiuka maalekezo haya”, alisema .Meneja wa Majaribio na Usalama wa Dawa, Bi. Kissa Mwamwitwa, aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA katika hotuba yake ya ufunguzi. 

Wadau hao pamoja na TFDA walikubaliana na kuweka maazimio kadhaa kwa lengo la kuwezesha zoezi husika kufanyika kwa ufanisi, miongoni mwa maazimio hayo ni kuanzisha chama cha wadau wa gesi tiba, kuboresha Mwongozo uliopo wa udhibiti wa gesi husika na watengenezaji wa bidhaa hiyo kuzalisha kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika ikiwa ni pamoja na kuweka maelezo ya kiusalama katika bidhaa zao kwa nia ya kulinda afya ya jamii. 
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa TFDA na wadau wa gesi tiba kutoka Serikalini na sekta binafsi nchini. waliokaa kutoka kulia ni Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA (wa pili), Meneja wa Vifaa Tiba, Vitendanishi na Vipodozi wa TFDA, Bi Grace Shimwela (wa tatu), Mwenyekiti mteule wa kikao hicho, Eng. Daudi Mlwale (wa kwanza) na Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
  Msajili wa Dawa Mkuu wa TFDA, Bi. Rose Aaron akisisitiza jambo katika mada aliyowasilisha mada.
Eng. Samwel Hayuma wa TFDA akiwasilisha mojawapo ya mada.
 Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akitoa hotuba ya ufunguzi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...