Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mabingwa watetezi wa michuano ya Kikapu ya Sprite Bball Kings, Mchenga Bball Stars wamefanikiwa kuondoka na ushindi wa kwanza katika hatua ya fainali, baada ya kushinda game 1 kwenye 'Best of five' dhidi ya wapinzani wao Flying Dribblers.

Mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa wiki huu kwenye uwanja wa taifa wa ndani uliweza kuwa wa ushindani mkubwa sana huku mabingwa watetezi wakitawala zaidi katika quarter zote nne na kufanikiwa kushindwa kwa pointi 103 dhidi ya 73 vya Flying Dribblers.

Mchenga walianza mchezo huo kwa kasi wakishinda quarter ya kwanza kwa pointi 27 dhidi ya 10 za Flying Dribblers kabla ya kuendelea kuongoza kwa pointi 62 kwa 25 hivyo kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa tofauti ya pointi 37. Katika quarter hizo mbili mchezaji Baraka Sadick alifunga pointi 32. 

Baada ya mapumziko Mchenga walirejea kwa kasi tena na kuongoza kwa pointi 62 dhidi ya 44 za Flying Dribblers. Mabingwa hao watetezi waliendelea na moto wao katika quarter ya 4 na kufanikiwa kufikisha pointi 100 ambapo hadi mwisho wa mchezo wakaongoza kwa pointi 103 kwa 73.

Katika mchezo huo mchezaji Baraka Sadick wa Mchenga Bball Stars ameibuka kinara wa jumla kwa kufunga pointi 48, Assist 6 na kuchukua rebound 4. Amefuatiwa na mchezaji Baraka Mopele wa Flying Dribblers ambaye amefunga pointi 29 na rebound 4.

Game 2 ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Sprite, itachezwa Jumatano Agosti 22, 2018 kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay. Mechi hizi zinaweza kwenda hadi game 5 endapo Flying Dribblers watarejea na kusawazisha katika game 2 na zinazofuata.

Mshindi wa mashindano hayo atanyakua kitita cha Shilingi Milioni 10 pamoja na Kikombe, Mshindi wa pili Milioni 3 na mchezaji bora MVP kupata milioni 2.
Mchezaji wa timu ya Flying Dribblers, Steve Mtemihonda (kushoto), akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa timu ya Mchenga Stars, Mohamed Yusuph, wakati wa mchezo wa kwanza wa fainali ya mpira wa Kikapu Sprite Bball Kings, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa ndani. Mchenga alishinda pointi 103 dhidi ya 73 za Flying Dribblers.
Mchezai wa timu ya Mchenga Stars, Baraka Sadick (kulia) akimiliki mpira huku akizongwa na wachezaji wa timu ya Flying Dribbers wakati wa mchezo wao wa kwanza wa fainali ya mpira wa kikapu Sprite Bball Kings uliofanyika Uwanja wa ndani wa Taifa Dar es Salaam. Mchenga alishinda pointi 103 dhidi ya 73 za Flying Dribblers.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...