Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (Kushoto)alitazama mwonekano katika picha wa Chuo cha Mkoa huo pindi kitakapomaliza.
Mwenyekiti wa Bodi wa Bodi ya VETA Ndg. Peter Maduki akikabidhi mchoro wa chuo cha VETA Geita kwa mkandarasi wa kampuni ya Skywards Construction aliyepewa kazi ya ujenzi wa chuo hicho
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Ndg.Peter Maduki wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Geita.Wengine ni Wakurugenzi wa VETA na wakandarasi wa mradi huo.
Uongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Chato, Uongozi wa VETA,Wakandarasi na baadhi ya wananchi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa chuo cha Wilaya hiyo kwa Mkandarasi.

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeanza utekelezaji wa  ujenzi wa Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Mikoa ya Geita, Njombe, Rukwa na Simiyu ikiwa ni sehemu ya kutoa huduma ya ufundi na ujuzi ili kukidhi mahitaji ya mikoa hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi maeneo ya ujenzi wa vyuo vya mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato, Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Peter Maduki  alisema  ujenzi wa vyuo hivyo kwa mikoa hiyo una lengo la kutekeleza mkakati wa Mamlaka wa  kuongeza udahili hadi kufikia idadi ya wanafunzi 700,000 ifikapo mwaka 2020.

Alisema kuwa jitihada hizo zinaenda sanjari na utekelezaji wa nia njema ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kuwa vijana wanapata ujuzi stahiki utakaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri ili kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi na kuhakikisha nchi inafikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Akikabidhi rasmi nyaraka za ujenzi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Mkoa wa Geita chenye ukubwa wa hekta 27 kwa Mkandarasi anayejenga chuo hicho Kampuni ya Kitanzania Skywards Construction
 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Maduki alisema kuwa gharama ya ujenzi wa chuo hicho ni kiasi cha Sh bilioni 9.9 fedha za mkopo kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...