Balozi Massuka akimkaribisha nchini Korea Bw.Adonis Bitegeko ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mwakilishi Wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA), moja ya taasisi muhimu za serikali zinazoshiriki katika ziara hiyo ya uhamasishaji viwanda nchini Korea. Anayeshuhudia ni Bw.Francis Mossongo, Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Tanzania.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Dawa na Vifaa Tiba Nchini (Tanzania Association of Phramaceutical Industry, TAPI), Bw.Abbas S.Mohamed, ambaye pia ni Mkurugenzi Wa Kampuni ya Samiro Pharmaceuticals Ltd ya jijini Dar es Salaam, akipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon Seoul na Mhe. Matilda S.Massuka, Balozi Wa Tanzania nchini Korea. TAPI inashirikiana na Serikali katika kufanikisha malengo ya ziara hiyo Nchini Korea na China, wakiiwakilisha Sekta Binafsi ya Tasnia ya Dawa na Vifaa Tiba ya nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe.Matilda S. Massuka, akimkaribisha Bw. Asgaral Alimohamed, Mwanachama Wa TAPI na Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni ya Mwafrika Pharmaceutical Ltd ya jijini Tanga, baada ya kutambulishwa kwake na Bw.Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC anayeongoza ujumbe wa Tanzania, nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Matilda Massuka akiulaki na kuukaribisha ujumbe wa Tanzania uliowasilini Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seoul Incheon, nchini Korea kwa ajili ya ziara ya uhamasishaji uwekezaji na biashara katika sekta ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania. Katika hatua ya awali, Ujumbe huo unaongozwa na Bw.Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, huku Ummy Mwalimu Waziri wa Afya wa Tanzania akitarajiwa kuungana na ujumbe huo nchini Korea mapema kesho kwa zaira ya kikazi ya siku tano (5) kuanzia Agosti 11 hadi15 mwaka huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...