Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

MKUU mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya amekemea vikali vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo hali iliyopelekea kutajwa kama mteja namba moja wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa( TAKUKURU) katika mkoa wa Kilimanjaro.

Sabaya pia ameinyooshea kidole idara ya Ushirika katika Halmashauri hiyo ambayo inatajwa kushindwa kusimamia vyama vya ushirika hadi kupelekea kuingia mikataba aliyoitaja kuwa ya hovyo na yenye kujaa rushwa.

Katika kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya wilaya kilicholenga kujitamburisha kwa watumishi hao Sabaya alisema Halmashauri hiyo inaongoza kwa ubadhilifu wa mali za umma na kwamba hadi sasa amepata taarifa za uwepo wa kesi nane zinazohusu rushwa.

“Mnaongoza kwa ubadhilifu na wa mali za umma,naambiwa kuna kesi nyingine zinaendelea na Takukuru inachunguza nyingine , hii ni aibu na ni fedheha kwa Halmashauri ,kama una mikono michafu hauna uhalali wa kumuubiri mtu habari njema niwaombe mbadilike”alisema Ole Sabaya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema zipo taarifa ya kuwa katika Halmashauri hiyo kuna baadhi ya watu wamejijengea tabia ya kutaka kuonekana kama miungu watu kwa kufanya maamuzi bal ya kuwashirikisha watu wengine huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Yohana Sintoo kulitazama hilo.

“Nimesikia wapo watu hapa ,wao mnakaa kwenye CMT(kikaocha ushauri ) mnafanya maamuzi yeye ni mungu mtu hapa ,ikifika wakati wa kutekeleza hawatekelezi ,mnawakatisha tamaa watumishi wengine walioko tayari kufany kazi ,walioko tayari kutekeleza yale tuliyoahidi wananchi tunategemea hao watu wabadilike”alisema Ole Sabaya.

 Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza kwa mara ya kwanza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya Hai katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. 

Mmmoja wa baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,akichangia jambo katika kutano wa Mkuu wa wilaya ya Hai na Watumishi wa Halmashauri hiyo. Katibu Tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wela akizungumza katika kikao hicho. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungumza katika kikao hicho. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...