Na Frankius Cleophace Tarime.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime Marwa Daud Ngicho amechagia Vifaa mbalimbali katika shule ya Msingi Mturu iliyopo Kata ya Turwa Mjini Tarime Mkoani Mara kwa ajili ya kuanzisha Stationery ya shuke hiyo kwa lengo la kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakipata katika kipindi cha Mtihani.

Mwenyekiti huyo ametoa Vifaa mbalimbali ikiwemo Mashine ya kutolea kopi Mitiani huku wazazi na walezi pamoja na wadau wa Elimu wakiunga Mkono harambee hiyo kwa kuchangia zaidi ya shilingi 70,000.Ngicho amesema kuwa ameamua kutoa vifaa hivyo kwa lengo la kuunga jitiada za serikali ya awamu ya tano katika kutoa elimu bure ili kila mtoto wakiwemo watoto wa maskini wanaenda shule.

“Nilipokea barua yenu ya mahitaji hayo yote sasa nimenunua vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi Millioni mbili na Laki Nne wajibu wenu ni kuvitunza ili kizazi na kizazi kiweze kunufaika” alisema Ngicho.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mturu Jumanne Obogo amesema kuwa gharama za kuandaa mitiani kipindi cha Mwaka mzima zilikuwa kubwa ambapo shule hiyo utumia kiasi cha shilingi Mill3.5 jambo ambalo ni changamoto kubwa , hivyo upatikanaji wa vifaa hivyo vitasaida changamoto hiyo hukua wakitoa shukrani zao. 

Pia Mwalimu huyo amesema kuwa licha ya shule hiyo kupatiwa vifaa hivyo bado inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa Matundu ya vyoo na kuomba Mgeni rasmi kuwasaidia kutatua changamoto hiyo ambapo baadhi ya wadau na wazazi katika harambee hiyo wameweza kutoa Mifuko ya Saruji pamoja na ahadi mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa Vyoo hivyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho akikabidhi moja ya kifaa kati ya Vifaa vilivyotolewa katika Shule ya Msingi Mturu kwa ajili ya kuanzisha Stationery Vyenye thamini ya Mill2.4 ikiwemo Mashine ya Kutolea Kopi Mitihani.
Wazazi na walezi wakiwa katika harambee ya kuchagia Vifaa vya Stationery katika Shule ya Msingi Mturu ambapo wazazi hao pamoja na walimu na wadau wa elimu wamechangia zaidi ya 70,000.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mturu Jumanne Obogo akibainisha changamoto mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho.
Baadhi ya Vifaa vilivyotolewa na Mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime Daud Marwa Ngicho vyenye thamani ya shilingi Mill 2.4.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...