NA LUSUNGU HELELA - MANYARA 

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewaagiza Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zake kuwashirikisha viongozi wa mikoa na wa wilaya wakati wanapokwenda katika maeneo yao kwa ajili ya kushughulikia migogoro ardhi kati ya Hifadhi na wananchi. 

"Nasema ni marufuku kwa Watumishi wa Wizara yangu kwenda kwenye maeneo ya Hifadhi bila kushirikisha uongozi wa eneo husika kwa jambo lolote litalohusisha wananchi na Hifadhi" amesema Mhe.Hasunga. 

Aliyasema hayo jana kwenye mkutano mkoani Manyara kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.William Lukuvi kwa ajili ya kuzindua utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na Hifadhi utakaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi. 

Mpango huo una lengo la kutatua migogoro ya ardhi kati ya wananchi na Hifadhi utakaoshirikisha mikoa mitano ya Manyara,Dodoma,Mara,Arusha na Simiyu kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi. 

Naibu Waziri, Mhe. Hasunga alitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo kwa awamu ya kwanza kuwa ni Manyara, Arusha na Mara yenye jumla ya vijiji 95 kati ya vijiji 392 vilivyolengwa nchi nzima. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wajumbe kwenye mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara -liowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na wajumbe wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (katikati) mara baada ya kufanyika mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. Wa tatu kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania, Martin Leibook.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanyika mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...