*Ni katika uzinduzi wa uwanja wa Halmashauri ya Ruangwa

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ruangwa kesho (Jumamosi, Agosti, 11, 2018) inatarajia kuzindua uwanja wake wa michezo, ambapo timu ya wilaya hiyo Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza itapambana na bingwa wa ligi kuu 2018/2019 Simba SC ya jiji Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Namungo FC ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini, imeupa heshima mkoa wa Lindi kwa kuwa ndiyo pekee inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa uwanja huo leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mbali na timu ya Simba pia timu hiyo inatarajia kucheza na timu za Yanga , Azam za jijini Dar es Salaam na Dodoma FC ya jijini Dodoma.Uwanja wa mpira wa miguu wa wilaya Ruangwa unaoitwa Majaliwa Stadium umejengwa katika kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea na ndio utakaokuwa unatumiwa na timu ya Namungo FC kuchezea mechi za nyumbani.

“Lazima tuisapoti timu yetu ya Namungo FC icheze daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”Kadhalika Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa timu ya Namungo FC kucheza na timu kama za Simba, Yanga, Azam na Dodoma FC kwa sababu zinasaidia katika kuimarisha viwango vya wachezaji na kuwaondolea uoga wa kupambana na timu nyingine.

Kiingilio katika mechi ya Namungo FC na Simba SC ni sh. 3000. Tayari timu ya Simba imeshawasili wilayani Ruangwa leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018), saa 11.01 jioni kwa ajili ya mechi yake na timu ya Namungo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na wachezaji wa Namungo FC, alipowatembelea kambini kwao Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 (Picha na  Ofisi ya Naziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akionesha jezi ya Namungo FC, baada ya kupokea jezi hizo zilizotolewa na wafadhili wa timu hiyo, Haojue Company Limited Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 Kushoto ni Mkurugenzi wa Haojue Brand Martin Francis. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wachezaji wa Namungo FC, alipowatembelea kambini kwao Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 (Picha na  Ofisi ya Naziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...