BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeingia makubaliano na taasisi ya umoja wa mataifa la maendeleo UNDP pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) na Taasisis ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii  (ESRF) kufanya tafiti mbalimbali zitakazo wezesha halmashauri za wilaya na mikoa kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwenye maeneo yao.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Bi.Beng’i Issa pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu  ESRF, Bi. Margareth Nzuki na Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Uchumi UDSM,Dkt. Kenneth Mdadila ambapo taasisi hizo kwa pamoja na UNDP watashirikiana kufanya tafiti hizo.

Bi. Issa alisema tafiti hizo zitasaidia halmashauri kutambua vipaumbele vyao katika  uzalishaji, kuandaa mpango mkakati utakaowezesha kutafuta fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo hususani kwa vijana.“ 

Kwa pamoja tumeamua kufanya hivi ili kuleta matokeo chanya ya tafiti na kusaidia jamii hususani katika  halmashauri zetu,” kazi za tafiti ni za kitaalam na tunataka zisaidie na hiyo ni njia muhimu katika kuunga mkono serikali ya awamu ya tano inayojenga uchumi wa viwanda, alisema Bi. Issa.

Pia alisema matokeo ya tafiti hizo pia yatasaidia baraza hilo kupata taarifa ambazo zitatumika kwenye utekelezaji wa mradi maalum wa miaka mitatu unaoratibiwa na baraza hilo kwa kushirikiana na umoja wa mataifa ambao utaanza mapema mwakani.

Alisema kazi hizo zinatarajiwa kukamilika kabla ya Desemba 2018 kwa kuwa nia ya ushirikiano huo ni kupata taarifa zitakazo tumika kuandaa andiko kubwa la mradi unaotakiwa kutekelezwa kwa miaka mitatu ijayo kati ya UNDP na baraza kuanzia Januari 2019.Alisisistiza kuwa tafiti hizo zitatoa taarifa ambazo zitawezesha kushughulikia zaidi uwezeshaji wananchi kiuchumi kulingana na makundi yanayolegwa.

Naye Mratibu wa mradi kutoka taasisi za kiuchumi na kijamii Magreth Nzuki, alisema utafiti huo utakapo kamilika  Utaleta mageuzi katika teknolojia ya kilimo kwa kuzalisha malighafi zitakazo hitajika kwenye viwanda.
 Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi (NEEC),Beng'i  Issa,akibadilishana nyaraka na Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa kufanya kazi kati ya baraza hilo pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
Katibu mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Beng'i  Issa,akibadilishana nyaraka  na Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt. Kenneth Mdadila, (kulia) baada ya kusain Mkataba wa kufanya kazi za tafiti kati ya baraza hilo pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na chuo hicho.


Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng'i  Issa katikati akisaini nyaraka ya makubaliano ya mkataba wa kufanya kazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP pamoja na Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF),  kushoto ni Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu ESRF,Bi. Margareth Nzuki na kulia ni Mwakilishi  wa Mkuu wa Idara ya Uchumi UDSM Dkt. Kenneth Mdadila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...