Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

 WAZIRI wa UJenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Isaac Kamwelwe amewataka watoa huduma wa ving’amuzi vya Azam, ZUKU pamoja na Multichoice kuendelea kutoa huduma zao za maudhui katika vituo vya televisheni bure kwa channel ambazo ziko katika leseni zao bila ya kuweka masharti. 

 Kamwelwe ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam kuhusiana na kadhia iliyojitokeza kwa watoa huduma hao. 
Amesema kuwa sheria na kanuni za nchi lazima zifuatwe kwa watoa huduma hao kutokana na masharti ya leseni walizopewa. 

 Amesema kuwa ving’amuzi vya Azam, ZUKU pamoja na Multichoice havijazuiliwa bali vitaendelea kutumika kwa mujibu wa masharti ya leseni zao walizopewa na mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Waziri wa Kamwelwe amesema utaratibu wa huduma za utangazaji kwa mfumo wa dijitali ulifikiwa baada ya maridhiano ya muda mrefu na wadau mbalimbali kwa waraka wa mashauriano na wadau hivyo lazima utaratibu uliowekwa uzingatiwe. 

 Amesema baada ya agizo hilo la serikali tayari Azam wametekeleza hivyo wadau wengine ambao walikuwa hawatoi huduma hiyo waendelee kutoa huduma bure kwa wananchi ili kupata habari katika vituo vya Luninga ambavyo vinatakiwa kurushwa bila malipo.
Waziri wa UJenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Isaac Kamwelwe akizungumza na waandishi habari kuhusiana na sintofahamu za ving’amuzi vya AZAM,ZUKU pamoja na Multichoice kususia utoaji wa matangazo ya Channel ambazo zinatolewa bure Jumamosi Agosti 11, 2018 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akifafanua jambo kuhusiana na hatua mbalimbali za TCRA itazozichukua kwa ving’amuzi hivyo ikiwa ni pamoja na ukiukaji wa leseni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...