Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

JUHUDI za Rais Dk.John Magufuli za kuleta maendeleo zimesababisha Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi(CUF), Julius Mtatiro kuamua kubadili gia aridhini kwa kujivua uanachama wa chama hicho.

Na kwamba amesema kuanzia leo atajikita katika kushiriki katika kufanya siasa za maendeleo na hasa kuunga mkono jitihada za Rais.Wakati anatangaza uamuzi huo ametaja sababu tano zilizomsukuma kufanya uamuzi huo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mtatiro ametaja sababu hizo ambapo ya kwanza ni kutoridhishwa na hali ya ushiriki na mchango wake kwenye siasa za CUF.Amesema sababu ya pili ni mgogoro wa kiuongozi unaoendelea kukikumba chama hicho na sababu ya tatu ni kutoridhidhwa na ushiriki wake kama kijana na kiongozi katika kuchochea maendeleo ya nchi.

Wakati jambo la nne likiwa ni ajenda ya maendeleo ya nchi, huku jambo la mwisho likiwa ni mustakabali wake kuhusu masuala ya siasa.

“Katika tafakari yangu ya kuhama, nilipitia maeneo kama matano ambayo nimefanyia kazi, niliangalia ushiriki na mchango wangu kwenye siasa za CUF, mgogoro unaoendelea kukikumba CUF, eneo la tatu ambalo nimelitafakari kwa upana sana ushiriki wangu kama kijana na kiongozi katika kuchochea maendeleo ya nchi, jambo la nne ajenda ya maendeleo ya nchi, la mwisho ni ustakabali wangu kuhusu masuala ya siasa,” amesema Mtatiro.

Mtatiro amesema ametumia muda wa mwezi mmoja kutafakari uamuzi huo, na kubaini kwamba huu ni muda wake wa kutumia talanta alizo nazo kumuunga mkono Rais John Magufuli kupitia CCM.
Aliekuwa Mwenyeki wa kamati ya uongozi wa chama cha wananchi CUF,Julius Mtatiro chini ya Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar as Salaam kuhusu na tarajio lake la kujiunga na chana cha Mapinduzi (CCM).Waandishi wa habari wakimsikilza aliyekua Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi wa chama cha wananchi CUF Julius Mtatiro (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...