Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

ALIYEKUWA katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Atta Annan (80) amefariki dunia leo katika hospitali ya Bern nchini Uswizi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kofi alikuwa  Mwafrika wa kwanza kutoka nchini Ghana kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na alihudumu kwa awamu mbili kuanzia Januari 1997 hadi Desemba 2016.

Baadaye alichaguliwa kuwa mmoja wa wajumbe katika kusuluhisha mzozo nchini Syria na alichangia katika kuleta suluhu.

Kofi Atta Annan alikuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa taasisi ya Kofi Annan na mwenyekiti wa wazee katika shirika la kimataifa lililoanzishwa na aliyekuwa Rais wa Afrika ya kusini Nelson Mandela.

Kofi alizaliwa  Aprili 8, 1938 huko Kumasi nchini Ghana na alisoma taaluma mbalimbali ikiwemo Uchumi aliyosoma katika Chuo cha Macalester na Uhusiano wa Kimataifa katika chuo cha Geneva ,Alianza kuitumikia UN mwaka 1962 katika shirika la afya Duniani  (WHO.) Na ameshinda tuzo mbalimbali ikiwemo ya kulinda amani 2001.

Kofi ameacha mke (bi Nane Maria Annan) na watoto (Kojo, Ama na Nina) ambao walikuwa karibu naye  hadi umauti unamfika.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Atta Annan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...