Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya Premier Bet imezindua mchezo mpya wa Football Jackpot utakaowapa fursa wateja wa kampuni hiyo kujinyakulia kitita kikubwa cha fedha cha Shillingi Milioni 15.5 za Kitanzania.

Jackpot hiyo iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Premier Bet, Samir Matar utakuwa mchezo wa kwanza wa Jackpot wenye kima kidogo katika michezo ya kubashiri nchini. Akizungumza na waandishi wa habari, Matar amesema kuwa Jackpot hiyo itakayohusisha mechi 12 za ligi mbalimbali droo yake itakuwa inachezwa kila siku ya Jumatano saa 3.55 usiku na Jumamosi saa 10.55 jioni. 

Ameeleza kuwa, wateja watatakiwa kubashiri mechi 12 zitakazokuwa zimeorodheshwa kwa mawakala wote nchini na atafanikiwa kushinda kitita hicho cha Milioni 15.5 na ikitokea mteja akabashiri mechi 10 au 11 atapatiwa fedha kulingana na ubashiri wake. 

Meneja Rasilimali watu na Utawala Amanda Kombe amesema kuwa lengo la kuanzisha Jackpot hii ni kwa ajili ya kukuza burudani ya soka kwa wateja wa Premier Football Betting ili kuwapa fursa ya kushinda kitita kikubwa cha fedha kwa kutoa hela kidogo. Amanda amesema, kama ikitokea katika siku ambayo Jackpot imechezeshwa mshinda wa Milioni 15 hajapatikana hivyo inapelekea kuongezeka kwa kiwango cha fedha.

Kwa sasa Premier Bet ina jumla ya mawakala 2000 nchini kote na ratiba za mechi zitakazokuwa zinashindanishwa zitakuwa zinapatikana kwa mawakala hao na mteja anaweza kucheza kadri ya uwezo wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Premier Bet, Samir Matar (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Football Jackpot   utakaowapa fursa wateja wa kampuni hiyo kujinyakulia kitita kikubwa cha fedha cha Shillingi Milioni 15.5 za Kitanzania.


Meneja Rasilimali watu na Utawala Amanda Kombe akiwaonyesha waandishi wa Habari aina ya tiketi ya michezo ya kubashiri ya Premier Bet wakati wa uzinduzi wa Jackpot ya Premier Bet Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Premier Bet wakionyesha namna ya kutoa risiti katika mashine kwa Mkurugenzi Mtendaji Samir Matar ( picha ya juu)  pia wakitoa tiketi kwa waandishi wa habari waliofika katika uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...