Akerwa na maamuzi kufanyika bila Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuarifiwa .Asema Wizara yake imeamua kubadili taswira ya Ofisi yake 

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuanzia sasa mawakili walioko kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wanasheria wote katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi za Serikali watakuwa ni Mawakili wa Serikali. 

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Agosti 15, 2018) kabla hajamkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ahutubie wageni waliohudhuria uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dodoma. 

“Kwa miaka mingi kumekuwa na ombwe la usimamizi wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma. Maamuzi mengi yamekuwa yakifanyika pasipo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuwa na taarifa. Mambo yanapoharibika ndio Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inataarifiwa ili kuokoa jahazi,” alisema. 

Alisema hali hiyo kwa miaka mingi imekuwa ikiisababishia Serikali kuingia kwenye migogoro na kuingia hasara. “Baada ya mabadiliko haya, wanasheria wote walioajiriwa katika utumishi wa umma wanakuwa wanafanya kazi na kutumia mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndani ya wizara zao, taasisi zinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za Mitaa,” alisema. 

“Vilevile wanasheria hao watakuwa chini ya uangalizi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nia ya mabadiliko haya ni kumuwezesha Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe na usimamizi juu yao na kuwazuia kufanya kazi bila kufuata maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...