Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Magufuli (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Uganda, Mh. Yoweri Museveni.

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni atafanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini tarehe 09 Agosti 2018.

Taarifa hiyo imetolewa leo 07 Agosti 2018 na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Uganda.

“Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Rais Museveni atapokelewa na mwenyeji wake Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Akiwa nchini, Mheshimiwa Rais Museveni atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mheshimiwa Rais Magufuli yatakayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yatafuatiwa na Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa heshima ya Mheshimiwa Rais Museveni.

Mheshimiwa Rais Museveni na Ujumbe wake wataondoka nchini siku hiyo hiyo kurejea Uganda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...