Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Ally Salum Hapi leo amefanya mkutano na wazee wa Mkoa wa Iringa ambapo wamemsimika rasmi kuwa Chifu wa wahehe, kama ishara ya kumpokea na kumpa nguvu ya kutawala mkoa wa IRINGA.

Katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa siasa ni Kilimo, wazee wa Iringa wamejitokeza kwa wingi kiasi cha wengine kukosa nafasi ya kukaa na hivyo kusimama na wengine mamia kuketi nje ya ukumbi huo.

RC Hapi alianza kwa kuwapa salamu za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli na baadae kutoa hotuba ya dira ya uongozi wake mkoani Iringa, vipaumbele vyake na kuwaomba ushirikiano wananchi wa Iringa.

"Mhe Rais amenituma niwape salamu zake. Lakini pia amenipa kazi ya kuhakikisha tunawatumikia na kutatua kero zenu ili wana Iringa mjivunie kuwa hamkukosea kumchagua Rais Magufuli na mjisikie fahari na nchi yenu. Siku zote nitasimama upande wenu wananchi na hasa wanyonge..."
Alisema Hapi

Katika hatua nyingine RC Hapi alitoa fursa wazee hao kueleza matarajio yao na changamoto zao ambazo wangependa serikali ya mkoa izifanyie kazi. Wazee wamemueleza RC Hapi changamoto za huduma zisizoridhisha hospitali ya Mkoa, majibu mabaya ya watoa huduma, migogoro ya ardhi, Maji na mikopo ya kina mama na ucheleweshwaji wa pembejeo kwa wakulima.



Aidha, wazee hao wakiongozwa na Kaimu Chifu wa Wahehe Mzee Gerald Malangalila wameeleza mkutano huo kuwa ni wa kihistoria kuwahi kutokea mkoani Iringa na wazee kujaa ukumbini hadi kukosa mahali pa kuketi.

"Mhe Mkuu wa Mkoa na ndugu wazee, sasa naweza kusema kuwa ile ziara ya Mhe. Rais alipokuja Iringa, mawazo yetu tuliyompa ameyafanyia kazi. Haijawahi kutokea kwa miongo mingi kiongozi akapokelewa kwa umati mkubwa wa wazee kama Huu hapa kwetu. Hii ni dalili kuwa kama ilivyo kwa Rais, nawe umeletwa na Mungu. Sasa tumekutawaza kuwa Chifu wetu, tutakutii, tutakupa ushirikiano na tutakulinda..."
Alisema Chifu Malangalila 

Akitoa neno la shukrani Mzee Agustino Mkini ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la wazee wa IRINGA alimshukuru Mkuu wa Mkoa na kumuahidi ushirikiano katika kujenga Iringa Mpya.

"Tunamshukuru sana Mhe Rais kwa kukuleta Iringa. Tunataka yale uliyokua unayafanya Kinondoni tukikuona, uyafanye Iringa..."
RC Hapi alimaliza kwa kula chakula pamoja na wazee wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Ally Salum Hapi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wazee wa Mkoa wa Iringa, mapema leo mchana.
 Sehemu ya wazee wa Mkoa wa Iringa, wakimsikiliza Mkuu wao wa Mkoa, Ally Hapi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...