Tukio maarufu la riadha la Rotary Dar Marathon ambalo hufanyika siku ya 14 Oktoba – siku ya Nyerere kila mwaka tangu 2009 litaadhimisha mwaka wa kumi tangu kuanza kwa tukio hilo.

Dhima ya Rotary Dar Marathon inaendelea kuwa "ponya maisha, badilisha jamii” na ni katika mwaka wa tatu tangu RDM imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za hospitali ya (CCBRT) kuwa na mradi wa hsopitali binafsi ili waweze kupunguza gharama ya hudua za ulemavu zinazotolewa na hospitali hiyo kwa wana jamii. 

 Fedha zote zitakazokusanywa mwaka huu kutokana na tukio la RDM zitakabidhiwa kwa CCBRT ili kukamilisha ujenzi wa kliniki hiyo binafsi na manunuzi ya vifaa husika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Rotarian Catherinerose Barreto, alisema kwamba kamati inayojumuisha wajumbe kutoka klabu nane za Rotary za jijini Dar es Salaam imeshaanza maandalizi kuhakikisha mwaka huu RDM inakuwa tukio ambalo ni la ubora wa hali ya juu. Aliongeza pia mlezi wa RDM Mheshimiwa Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi atakuwepo na kushiriki matembezi ya siku hiyo.

Tukio la Rotary Dar Marathon (RDM) licha ya kulenga lengo msingi la kuchangisha fedha kusaidia shughuli mbalimbali ili kuboresha ubora wa maisha kwa jamii zetu pia linahakikisha kutoa tukio lenye ubora wa kimataifa na la kufurahiwa na wanaoshiriki katika mbio au matembezi.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Catherinerose Barretto (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Hawa Mkwela akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu ambapo pia Rotary Dar Marathon itasheherekea kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2008.
Mwenyekiti wa bodi ya Rotary Dar Marathon, Sharmila Bhatt akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza maandalizi ya mbio na matembezi ya hisani ya Rotary Dar iliyofanyika wikiendi hii jijini Dar es salaam. Mashindano hayo yanatarajia kutimua vumbi, Oktoba 14 mwaka huu. Rotary Dar Marathon inatarajia kuwavutia washiriki 16,000 kwa mwaka huu.
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon wakifurahia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wikiendi hii jijini Dar es Salaam ambapo walitangaza rasmi maandalizi ya matembezi hayo kwa mwaka huu yanayotarajiwa kufanyika tarehe Oktoba 14, mwaka huu. Mbio za Rotary Dar zitaanza na kuishia katika viwanja vya ‘The Green’, Oysterbay.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...