Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekabidhi  Pikipiki ishirini na saba (27) aina ya Honda kwa Maofisa elimu kata  kutoka kata zote ishirini na saba (27)  za Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mkoani Iringa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri David William, amesema Pikipiki hizo zimefika kwa wakati muafaka ili kurahisisha jukumu la ufuatiliaji na usimamizi wa elimu katika Halmashauri.
“Mmepata usafiri huu ambao utachangia kutatua changamoto za kufanya kazi zenu hivyo, hatutaki kuona utoro unaendelea, hatutaki kuona mimba zinandelea hasa katika shule za sekondari, sasa hatuna sababu ni lazima tuhakikishe elimu inakua bora zaidi na ufaulu wetu kitaifa kama Halmashauri unapanda” alisema Mhe William.
Aidha, Mhe. William, ametoa wito kwa Maofisa elimu kata kuhakikisha wanazitunza Pikipiki hizo na kusisitiza kwamba usafiri huo sio kwa ajili ya kufanyia biashara ya bodaboda bali zifanye kazi iliyokusudiwa.
Pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Maafisa Elimu Kata Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William (kushoto)  akizindua pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Maafisa Elimu Kata. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina na anyefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Issaya Mbenje.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...