Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amekabidhi mashine 10 za kufyatulia matofali kwa jeshi la magereza la mkoa wa Lindi na kuwataka kuzitumia ipasavyo ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwemo makazi duni.

Mashine hizo ni sehemu ya ahadi aliyoitoa mwaka mmoja na nusu uliopita baada ya kufanya ziara katika mkoa wa Lindi. Masauni alikabidhi mashine hizo katika gereza la Lindi mjini mkoani hapa na kuwataka jeshi la magereza kujipanga ipasavyo namna ya kuzitumia ili ziwe na tija na manufaa kwao.

Alisema mwaka uliopita alifanya ziara ya kukagua shughuli za magereza na kukutana na changamoto mbalimbali ikiwamo makazi duni ya nyumba za udongo hasa katika gereza la Lindi Mjini. “Nawakabidhi mashine hizi leo, natarajia kuona mabadiliko yenye tija kutoka kwenu. Mkifanya vizuri nitawatafuta wadau wengine kwa ajili ya kuongeza mashine hizi,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;

“Nataka gereza la Lindi Mjini liwe la mfano kwa magereza ya mkoa huu. Tumieni nguvu kazi ya wafungwa mlionao kwa ajili ya kuboresha makazi yenu,” alisema Masauni. Alisema atalishangaa jeshi la magereza endapo hawatumii ipasavyo nguvu kazi ya wafungwa wakati wana changamoto mbalimbali zinazowakabili na njia za kuzitatua zipo wazi. 

Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), baada ya kupokea mashine kumi za kufyatulia tofali ambapo ni mpango maalumu wa Serikali kuondoa changamoto za makazi ya askari magereza nchini.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Shaibu Ndemanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipima ukubwa wa tofali lililofyatuliwa na moja ya mashine alizokabidhi kwa uongozi wa Gereza la Mkoa wa Lindi ikiwa ni mpango maalumu wa kuondoa changamoto ya makazi kwa askari magereza nchini. Wanaoshuhudia ni viongozi wa gereza hilo wakiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange (kulia). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Magereza mkoani Lindi. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...