WANANCHI wa Kijiji cha Daraja mbili katika kata ya Namwinyu wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameahidi kutoa ardhi bure kwa ajili ya
matumizi ya Chuo cha kilimo (SUA) ikiwa ni kivutio kwa chuo hicho kuharakisha ukamilishaji wa shughuli zake.

Ahadi hiyo ilitolewa na wananchi hao katika hafla fupi ya makabidhiano ya majengo yaliyo kuwa kambi ya wakandarasi wa shauri wa kampuni iliyojenga barabara kwa Kiwango cha lami Kilimesera-Matemanga.

Wananchi hao wamefikia uamuzi huo kwa tamko hilo kwa pamoja katika mkutano huo wakiwa wanajibu kauli mbali mbali za viongozi.Ambapo walisema kuwa mbali na mkutano mkuu wa kijiji hicho wapo tayari kutoa zaidi ya hekari 500 kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho na kwamba wapo tayari kuongeza endapo kutakuwa na mahitaji zaidi.

Kauli hiyo ambayo pia ilisisitizwa na Diwani wa Kata hiyo Thabiti Said walisema kuwa ujio wa chuo hicho katika eneo la kijiji chao kutasaidia kupanua kujengeka kwa Kijiji, kuharakisha maendeleo pamoja na kuwasaidia kuelimisha ndugu, jamaa na watoto wao hali itakayo wafanya kuanza kulima kilimo cha kisasa.

Awali Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Raphael Chibunda amewaeleza wananchi hao kuwa katika utekelezaji huo, Chuo hicho ambacho endapo watakipokea kwa kupeleka wanafunzi wengi kila mwaka kitakua haraka na kuwa chuo kinacho jitegemea katika kipindi kifupi kijacho.

Prof. Chibunda amebainisha kuwa katika utelekezaji huo chuo kimejipanga kuanza Oktoba mwaka huu kwa kutoa mafunzo katika nyanja za utalii, teknolojia na kutunza kumbukumbu."Ila baadae kitajitanua na kuongeza kilimo utaalamu wa vipando, Ugani, lishe,Tiba za wanyama, uzalishaji

wa Lishe ya Wanyama, Ufugaji wa samaki, sayansi ya utunzaji wa mazingira, misitu na wanyama pori, kilimo biashara pamoja na mafunzo ya maendeleo ya vijiji," amesema.

Amesema katika kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinaanza haraka na kuleta tija kwa wananchi wa maeneo hayo Chuo hicho kimepanga kupeleka trekta moja kati ya marekta 10 waliyokabidhiwa na Rais Dk.John Magufuli hivi karibuni na kuanzisha mashamba darasa ambayo yatasaidia wananchi wengi kwenda kujifunza kwa vitendo.

Kwa upande was Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkwanda Sudi amesema kuwa katika utekelezaji huo kwa kuanzia wananchi hao wamekubaliana kutoa hekta tisa na majengo 11 ambayo yalitumika na wakandarasi washauri wakati wa ujenzi wa barabara ya lami.

Mbunge wa jimbo la Tunduru kusini Daimu Mpakate amesema kuwa ujio wa Chuo hicho ni ukombozi wa wananchi waishio mikoa ya pembezoni ikiwemo Wilaya ya Tunduru pamoja na wilaya zilizopo katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amewataka wananchi kujipanga kwa kupeleka watoto wao Shule na kuhakikisha wanafaulu vizuri ili chuo hicho kiweza kuwanufaisha wakazi wa Tunduru, Namtumbo na watanzania wote kwa ujumla.

Amesema kwa vile Chuo kipo Tunduru itapendeza endapo kutakuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaotoka ndani ya wilaya ya Tunduru na wengine maeneo ya jirani kama Namtumbo, Nanyumbu, Masasi na Tanzania kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera pichani kulia akipiga makofi kuashiria furaha ya makabidhiano ya majengo hayo ya chuo ndani ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera  (kushoto) akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA ,Profesa Raphael Chibunda .
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera pichani kati akisoma moja ya taarifa kabla ya makabidhiano ya majengo hayo ya chuo cha SUA ndani ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...