TAASISI ya uhifadhi na Utalii ya Friedkin Conservation Fund, imetoa msaada ya shilingi milioni 110 ili kusaidia ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Vipaji maalum mkoani Simiyu. Msaada huo, ulikabidhiwa jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka na wakurugenzi wa taasisi hiyo wakiongozwa na Abdukadir Mohamed katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Nyakabindi Wilaya ya Bariadi.

Mohammad alisema taasisi yao ambayo inamiliki kampuni za Uwindaji na upigaji picha za kitalii, Mwiba Holdings Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris, ambazo zimewekeza mkoani humo, zimetoa msaada huo kusaidia watoto kupata elimu.Alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ya kusaidia jamii inayotolewa ili kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Simiyu kiujumla.

"Tunachoomba ni kupewa ushirikiano tufanye kazi zetu za utalii katika pori la akiba la Makao na Maswa na kuondolewa uvamizi," alisema.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alishukuru kwa msaada huo wa shilingi milioni 110 ambazo zitasaidia ujenzi wa shule hiyo.Alisema Taasisi ya Friedkin imekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo katika mkoa huo kwani hivi karibuni ilitoa msaada wa mifuko 3000 ya saruji na bati 1000 kusaidia elimu pia.

Kulikuwepo na migogoro katika eneo la mwekezaji huyo hivyo kabla ya kupokea misaada ya Saruji na bati Mkuu huyo wa mkoa aliongea na Rais Dk. John Mafuguli kuomba idhini ya kupokea."Niliona ningepokea mwenyewe maneno yangeanza ya kuchafuana, hivyo niliomba ridhaa ya Rais na akasema hii ni michango ya maendeleo tupokee. Mh. Rais alisema na shule ikijengwa wanaweza hata kuiita Mwiba," alisema.

Alisema licha ya msaada huo, taasisi hiyo imesaidia kutoa mchango wa ajira na imekuwa ikilipa kodi.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dk. Joseph Chilongani alisema Serikali inatambua mchango wa taasisi hiyo kwa maendeleo ya jamii.Alisema licha ya misaada inayotolewa ngazi ya mkoa, taasisi hiyo kila mwaka inatoa zaidi ya shilingi milioni 610 kama kodi ya pango na sehemu ya mapato ya utalii kwa vijiji 10 vilivyopo eneo la hifadhi ya jamii ya makao.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mkoa wa Simiyu, Gungu Silanga alisema Serikali ya CCM itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo kwani inachangia utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi."Miaka ya nyuma kulikuwa na watu wachache walitaka kutugombanisha lakini sasa chama na Serikali tupo pamoja kufanya kazi na wawekezaji Mkoa wa Simiyu,” alisema.Alisema.
Mmoja wa wakurugenzi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund,(FCF) Abdukadir Mohammed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (katikati) Anthony Mtaka akipokea hundi ya shilingi 110 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya vipaji maalum Mkoa wa Simiyu jana katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo na Mifugo, Nyakabindi Mkoa wa Simiyu. 
Mmoja wa wakurugenzi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund,(FCF) Abdukadir Mohammed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (katikati) Anthony Mtaka akipokea hundi ya shilingi 110 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya vipaji maalum Mkoa wa Simiyu jana katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo na Mifugo, Nyakabindi Mkoa wa Simiyu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...