Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika mjini Windhoek, Namibia, kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti 2018, umemteua Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha Agosti 2018 mpaka Agosti 2019. 

Kufuatia uteuzi huo, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapewa rasmi jukumu la Uenyekiti wa SADC katika Mkutano mkuu ujao wa 39 utakaofanyika Tanzania mwezi Agosti 2019. 
Makamu wa wa Rais Mhe .Samia Suluhu Hasan akitoa hutuba ya kushukuru mara baaada ya Tanzania kukabidhiwa Umakamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika - SADC katika ukumbi wa Mikutano katika hoteli ya SAFARI COURT ,Windhoek Namibia,leo Jumamosi tarehe 18 Agosti 2018.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini moja kati ya nyaraka nne za kisheria ambazo ni Tamko la Kutokomeza Malaria katika ukanda wa SADC, Itifaki ya Kulinda Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina mpya za Mbegu za mimea katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, itifaki ya ajira na kazi pamoja na Maboresho ya Katiba inayosimamia masuala ya kamati Ndogo ya Wakuu wa Polisi katika Organ.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa kwenye siku ya mwisho ya mkutano wa 38 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo mjini Windhoek Namibia ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha Agosti 2018 hadi Agosti 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda, Mhe. Cyril Ramaphosa akikabidhi nafasi ya Uenyekiti kwa mwenyekiti mpya na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Hage Geingob. 
Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akihutubia mara baada ya kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa SADC mjini Windhoek, Namibia ambapo aliishukuru Serikali ya Afrika kusini kwa uongozi mahiri kwa kipindi chote cha uongozi wake na aliahidi kushirikiana na wanachama wote katika kuiletea kanda maendeleo na kupunguza umasikini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...