SHIRIKA la Mawasiliano nchini (TTCL), limeahidi kutoa gawio kubwa zaidi kwa serikali mwakani, ili fedha hizo zikasaidie katika kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege vya serikali.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba ambaye alitembelea banda la maonesho ya Kilimo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, amesema wingi huo wa fedha utatokana na mashirika na taasisi za umma kuwaunga mkono kwa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.
“Mwaka huu tulitoa gawio la sh. Bil 5.1 kwa serikali, lakini ninaimani mwakani tutatoa zaidi endapo tutapata ushirikiano wa kutumiwa kwa huduma zetu kutoka kwenye taasisi nyingine za serikali, ambapo fedha hizo zinasambazwa na serikali kwenye kazi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa viwanja vya ndege,” amesema Bw. Kindamba.
Bw. Kindamba ameishukuru TAA kwa kuanza kutumia huduma ya mawasiliano ya simu kutoka kwenye shirika hilo, ambapo itasaidia kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi.  
Amesema anaahidi kuimarisha ushirikiano na TAA, na wapo tayari kutumia huduma zinazotolewa na mamlaka kwa maslahi ya nchini, ili kuimarisha na kukuza uchumi wa nchi.
“Ushirikiano wetu utasaidia kuongeza mapato, ambapo kila taasisi moja itaweza kutumia huduma na bidhaa za taasisi nyingine, kwa lengo la kuzifanya ziendelee kukua na kuimarika kiuchumi, kwani taasisi za umma zinategemeana zenyewe kwa zenyewe,” amesema.
Pia ameipongeza TAA kwa jitihada zake za kujitangaza kwa wananchi, ambapo ameitaka kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kujitangaza, naomba muendelee kuboresha viwanja vya ndege kwa maslahi ya Watanzania wote, kwa kweli najivunia sana uwepo wenu katika Nanenane “I am proud of your success’ na kweli mna iunganisha Tanzania kwa Ulimwengu,” amesema Bw. Kindamba.
  1. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (mwenye suti nyeusi) hivi karibuni akiongea na Kamati ya maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Afisa Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Edward Kimaro alipotembelea banda la Maonesho ya Kilimo na sherehe za Nanenane la Mamlaka, yanafanyika kwenye Uwanja wa Nyakabidni mkoani Simiyu.

 Baadhi ya wanakamati ya maonesho ya Kilimo na sherehe za Nanenane ya Mamlaka ya Viwanja wa Ndege Tanzania (TAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) (mwenye suti).
 Afisa Biashara na Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Herieth Nyalusi (kulia) akitoa maelezo ya ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha Mkoa wa Simiyu kwa Bi. Grace Kenedy (kulia) na Bi.Magreth Lend wakazi wa Bariadi, walipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa Nyakabindi.
Raia wa China wanaofundisha kwenye shule ya ya sekondari ya J.W.Bukanga Musoma, Bi. Jane Lee (wapili kushoto) na  Bi. Cary Zhang (watatu kushoto) wakimsikiliza Afisa Usalama Mwandamizi wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Bakari Mwalwisi alipokuwa akitoa maelezo kuhusu vimiminika kwenye banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi, mkoani Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...