Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Halima Mdee kwa tuhuma za kutoa lugha chafu ya matusi kwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli akiwa nyumbani kwa wazazi wake.

Ameeleza kuwa, walipofika nyumbani kwa wazazi wa Mdee Ubungo Kibangu, alipokelewa na mama mzazi yake zazi ambaye baada ya kujitambukisha na mahojiani mafupi aliwaeleza wamsubiri Halima anajiandaa kwa kuwa alikuwa amepumzika kidogo.

Mrakibu Kasanga ambaye ni shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka ameeleza hayo leo, Agosti 9,2018 wakati akitoa ushahidi dhidi ya kesi ya lugha ya matusi inayomkabili Mdee.Mdee anadaiwa, Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chadema,, alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.

Akiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amedai Julai 4, mwaka Jana, akiwa katika kituo cha polisi cha urafiki akiendelea na majukumu yake ya kawaida alipokea oda kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni Mark Njela akimtaka kwenda nyumbani kwa wazazi wa Mdee Ubungo Kibangu kumkamata Halima Mdee kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya rais Magufuli.

Amedai baada ya kupewa oda hiyo, walikwenda kama walivyoagiza na walipofika walipokelewa na kaka wa Halima ambaye aliwaelekeza kwa mama yao.Ameendelea kudai kuwa, mama Halima aliwapokea vizuri, akaenda kuongea na Halima na akaomba wamsubiri ajiandae kwa kuwa alikuwa amepumzika kwa kidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...