Na Mwandishi Maalum, Tanga

Serikali imezitaka Wizara na Taasisi za Umma kuhakikisha zinawajibika kikamilifu kufuata hatua zote muhimu za utekelezaji wa miradi ya Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partinaship-PPP), kwa kuwa hatua hiyo itaiwezesha Serikali kupata miradi ya maendeleo yenye sifa na ubora unaotakiwa nchini.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Said alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwa Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Taasisi na Mashirika ya Umma nchini.

Alisema kuwa utaratibu huo wa PPP ni njia bora ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kibajeti na kuiwezesha Serikali kuweza kufikia malengo yake katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kutoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi wake. 

Mhandisi Zena aliongeza kuwa, iwapo Halmashauri nchini zitafuata utaratibu wa PPP kwa kubuni miradi yenye sifa stahiki na kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango itasaidia kufikia malengo yake ya kujitegemea.

“Kiukweli hili ni jambo la faraja na ni fursa kubwa kwa Halmashauri zetu kutumia utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii hususani ujenzi wa hospitali za kisasa, miundombinu iliyobora”alisema Bi. Zena.Mhandisi Zena alifafanua kuwa Tanzania tayari imenufaika na uwekezaji kwenye miradi ya PPP kwa kuhusisha jumla ya miradi 20 yenye thamani ya Dola za marekani Milioni 863. 39.

Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said, akifungua mafunzo ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafisi katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa Tanga ulio jumuisha watendaji mbalimbali kutoka Halmashauri 60 nchini. 
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said, akisalimiana na mwezeshaji wa mafunzo ya ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi Bw. Node Ned White kutoka Benki ya Dunia, katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. 
Kamishna wa masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya akitoa maelezo mafupi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) kabla ya kumkaribisha kwa ajili ya ufunguzi wa mafunzo ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa Watumishi wa Halmashauri mkoani Tanga. 
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said, (wa pili kulia), (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa masuala ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya, (wa kwanza kushoto) ni Afisa Sheria Mkuu wa PPP Bi. Flora Tenga (wa pili kushoto) ni Bw. Hemedi Mpili kutoka TAMISEMI wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...