Dar es salaam  

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge amewataka viongozi wa hospitali hiyo kuwajibika na kutekeleza mikakati ya hospitali ipasavyo ili kufikia malengo iliyojiwekea.

Prof. Majinge ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokua akifungua mafunzo ya utawala bora yaliyohusisha Wajumbe wa Bodi, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara pamoja na Mameneja majengo wa hospitali hiyo.

Prof. Majinge amesema viongozi wanatakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kufikia malengo ambayo hospitali imejiwekea, lakini pia hatua hiyo itakua chachu kwa watendaji wa chini kufanya kazi kwa bidii.Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo amesema yana maana kubwa katika taasisi kwa kuwa yatasaidia kukamilisha mpango mkakati wa hospitali bila kuwepo na vikwazo.

‘’Safari ni ndefu ili kufikia malengo, Bodi ya wadhamini MNH na Menejimenti lazima tuwe kitu kimoja na tukubaliane mipango inayotakiwa kutekelezwa ili tusonge mbele hivyo wote kwa pamoja, lazima tuwajibike ili tutoe huduma bora,’’amesema Prof. Majinge.

Aidha mtoa mada katika mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) Dkt. Kassim Hussein amewataka viongozi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuwa na uongozi unaoacha alama.‘’Unapokua kiongozi lazima uwe mfano na watu watambue uwepo wako kwa kufanya kazi, uwepo wako katika taasisi uwe wenye tija,‘’ amesema Dkt. Hussein.

Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zimetolewa ikiwemo, utawala bora, mamlaka na wajibu wa bodi pamoja na wajibu na majukumu ya Wakurugenzi katika taa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wakurugenzi, wakuu wa idara, wakuu wa vitengo na mameneja wa majengo wa hospitali hiyo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru na Mjumbe wa Bodi ya hospitali hiyo, Juma Muhimbi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Mtoa mada kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania, Dkt. Kassim Hussein akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo leo.
Baadhi ya wakurugenzi na viongozi wengine wa hospitali hiyo wakifuatilia mafunzo hayo leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...