Viongozi na Watumishi nchini wamekumbushwa kutanguliza mbele moyo wa uzalendo na masilahi mapana ya taifa wanapotekeleza majukumu yao ili kupeleka maendeleo ya taifa mbele na kuimarisha usalama wa taifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akifunga kozi fupi ya tano kwa viongozi iliyofanyika Chuo cha cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania (NDC) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mkuchika amesema, ni matumaini kuwa washiriki waliohudhuria kozi hiyo, utendaji wao wa kazi utabadilika kwa kuwa na tija kwani sasa mbinu zote zinazohusu namna ya kufikiri kimkakati, kufanya tathmini katika mambo mbalimbali ili kufikia maamuzi wamezipata.

“Sasa mnatambua dhana ya usalama wa Taifa vema na kwa mapana zaidi, si kulinda mipaka na mali za wanajamii tu, bali pia inahusisha kutunza mazingira, kuwa na chakula cha kutosha, kupiga vita rushwa na madawa ya kulevya na mengine mengi ambayo ninyi mnayafahamu zaidi,” Mhe. Mkuchika amesema na kuongeza kuwa usalama wa watu ni muhimu kuliko jambo jingine lolote, hivyo masuala ya usalama yawe ni sehemu ya kuzingatia katika utendaji wa kila siku na hasa pale maamuzi yanayogusa masilahi ya nchi na jamii yanapotolewa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea zawadi ya tai, kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua kozi fupi ya tano ya Viongozi, iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimtunuku cheti Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James baada ya kuhitimu kozi fupi ya tano ya Viongozi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na washiriki wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira akitoa neno la shukrani baada ya kuhitimu kozi fupi ya tano ya Viongozi katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...