Na Mwandishi Maalum, Dodoma 

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, inakusudia kujenga Chuo cha aina yake kwaajili ya waendesha mashtaka nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo na ujuzi wa uendeshaji wa kesi na mashauri ya jinai.

Mkurugezi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, (DPP) Bw. Biswalo Mganga amesema Chuo hicho kitajengwa eneo la Usagara. Jijini Mwanza ambako tayari hekta 25 zimeshapatika kwaajili ya ujenzi huo.

Kwa Mujibu wa DPP ujenzi wa Chuo hicho unatokana na ukweli kwamba, hakuna chuo chochote kinachotoa mafunzo ya uendeshaji na usimamiaji wa kesi za jinai na kwa sababu hiyo Ofisi yake imeona kuna haja na umuhimu wa kuwapo kwa Chuo hicho.

Alikuwa akizungumza wakati hafla ya uzinduzi wa ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, uliofanywa mwanzoni mwa wiki hii, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jijini Dodoma

“Mhe. Waziri Mkuu, moja ya mikakati na mipango tuliyonayo ni kujenga chuo cha aina yaka katika Afrika ya Mashariki kitakachotoa mafunzo na namna ya kuendesha kesi za jinai. Tumeshapata hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekta 25 eneo la Usagara Mwanza kwaajili ya ujenzi wa chuo hicho”. Amebainisha Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka.





 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Bw. Biswalo Mganga akisalimia na Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  muda mfupi kabla ya  Waziri Mkuu kuzindua Ofisi  ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tukio lilofanyika kati kati ya wiki Jijini Dodoma. Katika taarifa yake DPP Mganga alieleza mpango wa Ofisi yake kujenga Chuo kitakachotoa mafunzo kwa Waendesha Mashtaka nchini. (Picha na  Habari  kwa hisani ya  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...