Wafanyabiashara Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kuondoa gharama za Cheti cha Matibabu na utaratibu wa Viza kwa nchi ambazo hazipo katika Jumuiya ya Afrika mashariki hasa kwa wafanyabiashara wadogo ili kuchochea biashara kati ya Mkoa huo na nchi jirani zikiwemo Burundi na Congo.

Hayo yamebainishwa Mkoani Kigoma wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, na Wafanyabiashara wa mkoa huo uliowakutanisha pia Madiwani wa Kigoma Ujiji na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na viongozi wengine.

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kigoma, Bw. Raymond Ndabhiyegetse, alisema kuwa Serikali imeweka gharama ya Viza ya Dola 50 na Dola 10 kwa ajili ya cheti cha chanjo kwa nchi ambazo si wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wadogo ambao ndio waliokuwa chachu ya biashara mkoani Kigoma.

“Waliobaki katika biashara ni wafanyabiashara wakubwa ambao hununua bidhaa za jumla kutoka viwandani na kusababisha wafanyabiashara wadogo wa mkoa wa Kigoma kutonufaika na kusababisha mzunguko wa pesa na biashara kuwa mdogo ikilinganishwa na kipindi ambacho hakukuwa na masharti ya kulipia viza na chanjo”, alisema Bw. Ndabhiyegetse.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiwaeleza wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji umuhimu wa kutoa lisiti na kulipa kodi, wakati changaoto za biashara na nchi jirani zikitatuliwa, alipofanya Mkutano na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo Mkoani Kigoma, wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Kassim Mchatta na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiwaeleza wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji umuhimu wa kutoa lisiti na kulipa kodi, wakati changaoto za biashara na nchi jirani zikitatuliwa, alipofanya Mkutano na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo Mkoani Kigoma, wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Kassim Mchatta na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko.
Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA) Bw. Baghayo Saqware, akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma kuhusu umuhimu wa Bima wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na wafanyabiashara hao.
Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zito Kabwe, akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya Kodi zinazotozwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...