NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE .

HOSPITAL ya wilaya ya Chalinze ,Msoga mkoani Pwani ,inakabiliana na changamoto za uzazi ambapo baadhi ya akinamama wamekuwa wakitumia dawa za mitishamba ili kujifungua haraka hali inayosababisha wakati wa kujifungua kuwa na uchungu mkali ,mtoto kuchoka na kutokwa damu nyingi. 

Mganga mfawidhi katika hospital hiyo Patricia Kihula ,alisema wapo akinamama wajamzito wanaoshikwa uchungu kisha kunywa mizizi ama dawa za kienyeji jambo ambalo ni hatari kwa mama na mtoto. Alisema kwasasa wanaendelea kutoa elimu katika klinik . 

Patricia alisema ,hali hiyo inasababisha mama akiwa tayari kanywa mizizi mchungu unakuwa mkali kabla ya njia kufunguka na mtoto kuchoka toka akiwa tumboni . “Tunatoa elimu kwa jamii wasiwe na tabia hiyo ,”na sisi tumeanza kupambana na tabia hiyo kwa kuwapa chai kabla ya kujifungua kwani tumegundua wanapewa dawa hizo ndani ya chai “. 

” Tumetoa maagizo chai inapaswa kutolewa kituoni hapa hapa ,na chai ikitoka nyumbani tunamwelekeza aliyeleta chai aanze kuionja ili kujiridhisha isiwe na dawa za kienyeji”alifafanua Patricia. Patricia alieleza kuwa , hakuna kesi ya kifo cha mtoto ama mama na badala yake zipo kesi mbili kila mwezi, za mama kuwa na uchungu mkali ,kutokwa damu nyingi au mtoto kutokwa kachoka sana . 

“Endapo inatokea mama kutokwa damu nyingi tunawapelekea hospital ya rufaa ya Tumbi kwa ajili ya upasuaji ili kuokoa maisha ya mama na mtoto na akitokwa damu nyingi pia huwa tukimchunguza kujua chanzo na hupatiwa matibabu” Patricia aliiomba akinamama wajawazito waache kutumia vitu,ama madawa ya majani,mitishamba ,dawa za kienyeji kwa kuweka kwenye njia ya uke ama kunywa bali wakisikia uchungu wakimbilie hospital kupata matibabu ya uhakika. 


Nae mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze, Rahim Hangai ,alisema wamepokea kesi za aina hiyo ambapo wameanza kutoa elimu ili kupunguza tatizo hilo . Alielezea ,wakitumia dawa hizo husababisha kupata uchungu wa kasi na kupasua kizazi ama mtoto akafa kabla ya kuzaliwa . Dk.Hangai alisema, dawa za kienyeji haziongezi uchungu ,waepuke madhara ambayo yataleta athari kwao. Mamamjamzito Hamisa Kheri alisema wengi wao wanajidanganya kutumia dawa hizo ili kuzaa haraka bila ya kuwa na uchungu kwa muda mrefu.

Mganga Mfawidhi hospital ya wilaya ya Chalinze Msoga,Patricia Kihula akitoa ufafanuzi wa jambo ,wakati mbunge wa Chalinze Ridhiwani alipokwenda kutembelea hospital hiyo .(picha na Mwamvua Mwinyi) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...