Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WAMILIKI wa visambusi(ving'amuzi)nchini wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kusimamia na kufuata sheria.

Pia wameishukuru bodi ya TCRA na Mkurugenzi wake mkuu kwa kusimamia sheria dhidi ya waendeshaji wa PAY TV ambao wamevunja sheria kuanzia mwaka 2010

Wakizungumza jijini Dar es Salaam baadhi ya wamiliki hao wa visambusi wameanza kwa kueleza kwanini TCRA walitupatia leseni ya MUX (Multiplexer).

Pia kwa nini ilikuwa lazima kuanzisha mfumo wa watoa huduma kwa ving’amuzi (MUX) katika sekta ya matangazo ya luninga na nini lilikuwa lengo la lesseni hiyo?

Hivyo wamefafanua kuwa katika kipindi  baada ya mwaka 2000, vyombo vya udhibiti vilianza kupata tatizo la upungufu wa masafa (frequency).

Na kwamba hilo  lilikuwa tatizo la dunia nzima, ITU na wadau wake wakakubaliana kuhamia katika masafa ya kidigitali, katika mfumo wa kianalogia unahitaji frequency moja kwa chaneli moja ya TV.

Wakati katika mfumo wa kidigitali frequency moja inaweza kusafirisha kati ya chaneli 15-18 za Televisheni kupitia technologia ya DVB-T, au chaneli 20-25 kupitia teknologia ya DVB-T2 kwa kutumia teknologia ya kupunguza ya DVB-T na T2.

Pia katika mpangilio mpya, watoa huduma za ving’amuzi wanatakiwa kutengeneza mtandao wa kusafirishia matangazo, na vituo vya televisheni vingetengeneaza maudhui ambayo yangebebwa na watoa huduma za ving’amuzi baada ya kukubaliana malipo.

Wamiliki hao wamesema watoa huduma za ving’amuzi wanatakiwa kuweka miundombinu kama dishi, vifaa vya umeme, ama nyaya za kusafirisha matangazo kwa nje.

Pia Gharama za uwekaji wa miundombinu hutegemea ubora na chapa ya vifaa hivyo, mara nyingi inagharimu mamilioni ya dola za kimarekani kuweka miundombinu hii.

Wamesema kwa kuongezea, watoa huduma za ving’amuzi wanahitaji kuweka miundombinu ya kurushia matangazo katika kila mikoa, gharama ya mtambo mmoja unagharimu fedha nyingi sana.

Hivyo hasara walizopata kwa kuruhusu visimbusi vya kulipia kubeba chaneli za Bure.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...