Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAMILIKI wa Viwanda vya Kuzalisha Saruji wamesema kuwa wataongeza uzalishaji wa saruji ili kuondoa hali ya upunguaji wa saruji nchini pamoja na kurudisha bei ya zamani ya saruji na sio ya 14000 pamoja na 15000.

Wamiliki wa viwanda vya Saruji waliyasema hayo wakati walipokutana na serikali kupitia Wizara ya Viwanda , Biashashara na Uwekezaji wakiongozwa na Najibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanaya walisema walikuwa na changamoto ya upatikanaji wa makaa yam awe pamoja na baadhi ya viwanda kuharibika Mitambo.

Akizungumza na wadau hao Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa wamiliki hao wazalishe saruji ya kutosheleza nchi kwanza na zaida ya saruji hiyo wauze nje ya nchi.Amesema kuwa kuuza saruji nje ya nchi ni fursa kiuchumi hivyo lazima viwanda vizalishe kwa kukidhi mahitaji ya ndani na ziada iuzwe nje, kuuza saruji nje na ndani kukawa na uhaba sio sawa.

Amesema kuwa wazalishaji wa makaa ya mawe wazalishe kwa wingi makaa hayo katika kuweza kulisha viwanda vya saruji pamoja na Tarula na Tanroad kujenga miundombinu sehemu yanakotoka makaa ya mawe.
Shirika la Taifa la Madini (Stamico) limesema kuwa litaongeza kasi katika uzalishaji wa makaa ya mawe katika miradi yake ya Kiwira pamoja na Kaburu ili kuhakikisha viwanda vya saruji vinapata makaa ya mawe ya kutosha.

Akizungumza na waandishi habari Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico , Alex Rutagwelela amesema kuwa kazi yao ni kuhakikisha wanalisha makaa ya mawe ya kutosha kwa wazalishaji wa saruji nchini.

Amesema kuwa changamoto ya viwanda vya saruji ni makaa ya mawe hivyo kasi ya uzalishaji lazima iongezeke katika kutatua tatizo la upungufu wa saruji usiwe kujirudia kwa mara nyingine kutokana na miradi mingi inayotekelezwa inahitaji saruji hiyo.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji wa Saruji katika mkutano wa kujadili upungufu wa Saruji nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Profesa Joseph Bushweishaija akitoa maelezo kuhusioana na mkutano na huo kwa wadau wa uzalishaji wa viwanda vya saruji.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico, Alex Rutagwelela akizungumza na waandishi habari kuhusiana na stamico iliyojipanga katika uzalishaji wa makaa ya mawe .
Baadhi ya wazalishaji wa viwanda vya Saruji nchini 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...