NA FREDY MGUNDA IRINGA.
Wananchi 2,587 wa kijiji cha
Lupembelwasenga Wilaya ya Iringa Vijijini wamekabidhiwa Hati za Hakimiliki ya
Kimila chini ya Mradi wa LTA Uliofadhiliwa na wadau kutoka Marekani wa Feed the
Future USAID.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Hati hizo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Makazi Angelina Mabula alisema kuwa katika miaka miwili ya utekelezaji,Mradi
huo umeweza kutoa jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 35,286 katika vijiji
26.Mabula alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi
mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya
ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.
Mabula aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi
kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo
itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.“Usajili wa
ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha
uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Mabula
Mabula aliupongeza mpango huo akisema utasaidia kupunguza eneo kubwa la ardhi
ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo haijapimwa.Aidha Mabula aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau
ufike umalize kupima vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa huku akivikumbusha vijiji vyote vya wilaya hiyo kuendelea
kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya
nchi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Angelina Mabula akikabidhi hati za kimira kwa wananchi wa kijiji cha Lupembelwasenga Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Angelina Mabula akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela,mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati pamoja na viongozi wa LTA wakati wa ugawaji wa hati za kimila
Picha ya pamoja.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...