Na Humphrey Shao, Globu jamii

Zaidi ya Wasichana 10,000 wamefikiwa na huduma zitolewazo na tasisi ya Msichana Initiative katika kipindi cha miaka Miwili na nusu tangu kuanzishwa kwake nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo , Rebeca Gyumi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kongamano la Ajenda ya Msichana linalo Taraji kufanyika Agosti 11 mwaka hu katika ukumbi wa Kisenga LAPF Millennium Tower Dar es Salaam.

Gyumi amesema kuwa kupitia kongamano hilo jumla ya Washiriki 1000 watashiriki wakiwemo wasichana walio ndani ya shule na nje ya shule kutoka klabu za Msichana Café na Makundi ya watu wenye mahitaji maalum.

“kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tangu kuanzishwa kwa tasisi hii tumeweza kuwafikia wasicha 10000 moja kwa moja hivyo katika mkutano wa mwaka huu 2018 tumekuja na kauli mbiu isemayo ‘Nafasi ya Jamii kwenye kuunda na kutetea haki za mtoto wa kike’ huku msisitizo mkubwa wa kauli hii mbiu ni kuangalia namna gani Wasichana wanazifahamu haki zao na kujua jinsi ya kuzitetea ili kuleta Mabadiliko chanya kwenye jamii” amesema Gyumi.

Gyumi alisema kuwa Mgeni rasmi katika kongamano hilo anataraji kuwa Mkurugenzi kutoka shirika la Women Fund Tanzania(WFT)Mery Lusimbi, aidha Wasichana watapata nafasi ya kuzungumzia changamaoto mbalimbali wanazozipitia .

Amesema taasisi ya Msichana Initiative ambayo inafanya kazi kwa ukaribu na serikali katika kupinga ndoa za utotoni , Unyanyasaji na ukandamizaji wa kijinsia kwa lengo la kuwapa nafsi wasichana kufikia malengo yanayotakiwa katika Maisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Kongamano la Ajenda ya Msichacha linalotaraji kufanyika agosti 11 mwaka huu katika ukumbi wa Kisenga LAPF Millennium Tower Dar es Salaam.
Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kutambulisha Kongamano la Ajenda ya Msichana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...