WATANZANIA hususani watoto na akina mama wajawazito wametakiwa kutumia zaidi mchicha nafaka kama chakula kitakachowaongezea viini lishe muhimu kwa afya ya miili yao. 

Wito huo umetolewa mjini Arusha wakati wa Kongamano la linalojadili Afya na na Lishe bora liliwakutanisha wataalamu wa masuala ya lishe kutoka ndani na nje ya nchi wakiwamo wanajamii. 

Kongamano hilo lililoanza Agosti 6 na kukamilika Agosti 9, Mwaka huu linafanyika hapa ambapo wataalamu wanabadilishana uzoefu kuhusu masuala ya afya na lishe bora limeandaliwa na Shirika la World Vission Tanzania (WVT), wakishirikiana na Taasisi ya Amaranth ya Marekani na ECHO. 

Akizungumza kwenye kongamano hilo Mkurugenzi wa Uendeshaji Miradi ya Shirika la World Vission Tanzania, Dk. Yosh Kaslima alisema kupitia shughuli wanazofanya kwenye mikoa 13 na wilaya 36 wamebaini kuwapo tatizo la lishe bora kwa watoto na mama wajawazito. 

“Wananchi hawajui wawalishe nini watoto na akina mama wajawazito, kwa hiyo tunatarajia kupitia kongamano hili washiriki watatoa na kupokea elimu mimea gani ina virutubisho vitakavyowawezesha kuboresha afya za watoto wakiwa wadogo,” alisema Kaslima. 

Kwa upande wake mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema, ujumbe wa kongamano hilo unaohamasisha lishe ni muhimu kwani umekuja kwa wakati sahihi. “Hii inakwenda sambamba na Sera ya Taifa ya Chakula na Lishe ya mwaka (2007) inayohamasisha uhusiano wa chakula na lishe katika sekta mbalimbali na utokomezaji wa utapiamlo hasa kwa watoto na kina mama,”

“Kumuelimisha kila mwananchi, aelewe kuwa ana wajibika moja kwa moja kutunza afya yake na ile ya familia yake. Kujenga ushirikiano kati ya sekta ya umma, sekta binafsi, mashirika ya dini, asasi za kijamii na jamii katika kutoa huduma za lishe na afya,” alisema Gmbo kupitia kwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega.
 Wataalamu wa masuala ya afya na lishe kwa mama na mtoto wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano la Kimataifa kuhusu Lishe katika maeneo kame nchii lililofanyika mjini Arusha 
Wataalamu wa masuala ya afya na lishe kwa mama na mtoto wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano la Kimataifa kuhusu Lishe katika maeneo kame nchii lililofanyika mjini Arusha katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...