Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WATEJA wa DStv wanatarajia kuanza tena kushuhudia moja ya ligi maarufu kabisa duniani ikiwemo Ligi ya Italia– Serie A.

Hatua hiyo inakuja baada ya MultiChoice kutangaza leo jijini Dar es Salaam kuwa kuanzia msimu huu, ligi hiyo itaonyeshwa mubashara kupitia DStv.Mbali na Serie A ambapo atakuwepo nguli wa soka Cristiano Ronaldo, wateja wa DStv wataendelea kufurahia ligi na michuano mikubwa mingi duniani ikiwemo Ligi ya Uingereza (Premier League) na La Liga.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema mbali na habari za kurudi kwa Serie A, DStv pia itaongeza maudhui zaidi katika soka msimu huu.Amesema watumiaji wa DStv Bomba, wataweza kuona zaidi ya mechi 100 katika michuano ya Serie A na Ligi Kuu ya Uingereza, huku wateja wa DStv Family wao watakuwa wakipata mechi zote 380 za michuano ya Serie A na mechi zaidi ya 120 kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.

Ameongeza kuwa watumiaji wa kifurushi cha DStv Compact, Compact Plus na wateja wa Premium watakuwa na upatikanaji wa mechi zote za Premium League, Serie A na mechi zote 380 za La Liga.Amefafanua kuwa wanatambua msimu wa ligi kwa mwaka 2018/2019 unatarajia kuanzia na kwa Ligi Kuu ya Uingereza inaanza Ijumaa hivyo rai yao kwa wateja wao kuhakikisha wanalipia ving'amuzi vyao na wale ambao hawana basi wanunue kwa gharama ya Sh.79,000 ikiwa na ofa ya miezi miwili.

Amesema kuwa lengo lao ni kuona wateja wao wote wanapata nafasi ya kuangalia ligi mbalimbali duniani pamoja na michuano mingine ya kimataifa.Ameweka wazi kuwa baada ya michuano ya Kombe la Dunia kumalizika sawa kwa nguvu ile ile wanahamishia kwenye ligi hizo ambapo mechi zitatangazwa kwa lugha ya kiswahili kupitia watangazaji na wachambuzi maarufu nchini.Shelukindo amesema katika vifurushi vyote vya Dstv wateja wataona mechi na kufafanua kwa vifurushi cha Sh.19,000 mteja wao atashuhudia mechi 108.Amesema kauli mbiu yao katika msimu huu wa ligi Kuu mbalimbali ni kwamba "Moto hauzimwi na kama sio DStv potezea".

Wakati wanatangaza kuanza kwa ligi na namna ambavyo DStv wamejipanga vema kwa ajili ya wateja mbali ya kuwepo kwa waandishi wa habari pia walikuwepo wachezaji mpira wa miguu maarufu nchini ambapo wamepata nafasi ya kutamba kwenye timu ya taifa na kwenye vilabu vyao.
Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo

Ephraem Kibonde mtangazaji maarufu wa Soka hapa nchini akizungumza (kutoka kushoto) Maulid Kitenge, Aboubakar Liongo, Edo Kumwembe wakiwa katika uzinduzi wa msimu mpya wa sokawatangazaji hao watakuwa wakiwaletea matangazo ya ligi kuu ya uingereza msimu huu kwa kiswahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...