MKURUGENZI mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio amewataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 na kwamba hatovumilia wazembe.

Erio aliyasema hayo jana katika mkutano wake na Wakurugenzi na Mameneja wa shirika hilo kwenye ukumbi wa NSSF Ilala Dar es Salaam.

"Mwaka jana mlipaswa kukusanya shilingi Trillion 1 lakini mlikusanya shilingi billion 700 pekee hivyo hamkufikia lengo." Mwaka huu katika mpango kazi ulioidhinishwa na Waziri mnapaswa kukusanya shilingi Trilioni 1.5 target hii lazima hifikiwe."alisema Erio 

Alisema fedha hizo zitapatikana kupitia uandikishwaji wa wanachama wapya, makusanya ya fealisema. wanachama wa zamani pamoja na fedha za pango za majengo ya shirika hilo."Hakuna haja ya kuwa na wanachama lukuki ambao hawalipi michango yao, ni lazima wafuatiliwe kwa karibu kuhakikisha michango inalipwa kwa wakati.

" Najua pia tuna majengo yetu ambayo yapo wazi hayana wapangaji, nimeshaongea na SSRA wanampango wa kufungua ofisi mikoa yote 26 ya Tanzania bara, wapange kwenye majengo yetu." alisema.Hata hivyo, Erio alisema kuwa hatomvumilia mfanyakazi mzembe ambae hatofikia malengo waliyojiwekea."Mkuu wa idara ambae hatofikia performance tuliyojiwekea sitomvumilia, naomba target tuliyoiweka ifikiwe, isipofikiwa maana yake kazi zmewashinda na Mimi sitokuvumilia." alisisitiza.

Erio alisema kuwa jukumu la kusajili wanachama wote ni la wafanyakazi wote na si idara moja pekee." Mwaka huu tunatakiwa kuandikisha wanachama wapya 417,000, NSSF inawafanyakazi 1,000 kila mfanyakazi akileta wanachama 10 kwa mwezi lazima watalipa michango na tutafikia lengo.

Akisisitiza hilo alisema malengo ya shirika yalifikiwa kwenye vikao halali vya wafanyakazi na muktasari ya yatokanavyo kwenye vikao hivyo upo, hivyo ni jukumu la kila mfanyakazi kutekeleza jukumu lake ili kufikia lengo la shirika ambalo ni kujiimarisha na kukua zaidi.

Hata hivyo kwa sasa anaendelea kusoma ripoti mbali mbali za utekelezaji alizokabidhiwa na mtangulizi wake pamoja na wakurugenzi wa kanda na kisha atafanya ziara ya kutembelea kila kitengo ili kubaini changamoto zilizopo miongoni mwa wafanyakazi na kuangalia namna ya kuziondoa.

Erio ambae awali alikuwa mkurugenzi wa PPF aliteuliwa Julai 14 mwaka huu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF akichukua nafasi ya Godius Kahyarara.
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio akizungumza na  Wakurugenzi na Mameneja wa shirika hilo kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam jana huku akiwataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 
 Baadhi ya Wakurugenzi na Mameneja wa shirika la NSSF  wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio ,alipozungumza nao jana kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam kuhusiana mikakati mipya ya kuimarisha zaidi mfuko huo,ambapo Watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 . 
 Sehemu ya Viongozi wakuu wa NSSF wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu William Erio ,alipozungumza nao jana kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam kuhusiana mikakati mipya ya kuimarisha zaidi mfuko huo,ambapo Watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...