NA LUSUNGU HELELA-DODOMA .

Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Lusius Mwenda ametoa wito kwa watumishi wa Serikali kuwa mstari wa mbele kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mapya ikiwa pamoja na kupumzisha akili. 

Pia amewataka watumishi hao kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio hivyo ili waweze kuona na kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo wanaweza kuanza kuzifanya kwa ajili ya kujiingizia kipato ikiwa ni njia mojawapo ya kuanza kujiandaa kwa ajili ya kustaafu. 

Amefafanua kuwa kila mtumishi wa Serikali anatakiwa kuanza kujiandaa kwa ajili ya kustaafu kuanzia ile siku ya kwanza aliyoajiriwa. Amesema watumishi walio wengi mara baada ya kustaafu hali zao za kiuchumi huteteleka kwa vile katika kipindi cha utumishi wao walikuwa hawatembelei maeneo tofauti na yale waliyoyazoea kwa ajili ya kujifunza na kukutana na watu tofauti. 

Ametoa Rai hiyo jana katika kituo cha utalii Kolo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma alipokuwa ameongozana na Watumishi zaidi ya 50 kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii , Ikiwa ni moja ya jitihada za Wizara hiyo kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali kwa kuanza na Watumishi wa Wizara yenye dhamana. Kivutio cha Utalii, Kolo kipo ni kivutio mashuhuri sana kwa michoro yake ya miambani kwa vile inafanana na michoro ya Afrika Kusini na kimebeba tamaduni za waafrika. 

” Tunataka Watumishi muwe mabalozi wazuri kuanzia kwenye ngazi ya familia hadi ngazi ya taifa kwa kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo maeneo ya kihistoria ambavyo yamesheheni chimbuko la tamaduni zetu pamoja na harakati za binadamu katika kupambana na mazingira yake.” alisema .

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Lusius Mwenda (kushoto) akiwa ameongoza na Watumishi zaidi ya 50 wa Wizara hiyo wakipanda kilima kwenda kuangalia michoro ya miambani katika kituo cha Utalii cha Kolo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma jana ikiwa lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali. Wa pili ni Mkuu wa Kituo cha Kolo, Zuberi Mabie. 
Mkuu wa Kituo cha Utalii, Kolo chenye michoro ya miambani, Zuberi Mabie akiwa na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwaonesha michoro ya miambani katika kituo cha Utalii cha Kolo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma jana ikiwa lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali.

Mkuu wa Kituo cha Utalii, Kolo chenye michoro ya miambani, Zuberi Mabie akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipotembelea kituo cha michoro ya miambani, Kolo kilichopo wilayani Kondoa wakati walipotembelea katika kituo hicho ikiwa la lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...