Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

WAZIRI wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Mkuranga katika kukagua utekelezaji wa utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi na hakuridhishwa na utendaji wa baadhi ya wahusika katika idara hizo na kuamua kuwaweka kando ili wenye kasi watekeleze jukumu hilo.

Katika Ziara hiyo Kalemani  amemuagiza meneja Tanesco  mkoa wa Pwani kumsimamisha kazi  Mhandisi wa Mkoa na  pia amemuagiza meneja wa wilaya ya Mkuranga Mhandisi, Regina Mvungi kumsimamisha mhandisi mwenye dhamana hiyo katika wilaya ya Mkuranga kwa kushindwa kufanya kazi ya kuwasha umeme kwenye vijiji vilivyo kwenye mradi kata ya Vikundi.

Aidha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ametoa siku 14 Wilayani Mkuranga katika  kuhakikisha umeme unawaka katika vijiji vyote vilivyokatika mpango huo.Waziri hiyo aliyasema hayo Leo hii wakati wa ziara ya kutembelea wilayani Mkuranga ili kuona namna ya upatikanaji wa huduma ya Nishati ya Umeme katika Kata ya Kisiju,Vikindu na Tambani.

Kalemani amesema kuwa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya pili haikufanya vizuri katika Tarafa ya Kisiju hivyo natoa siku 14 kuanzia kesho kuhakikisha umeme unawaka, aidha Kalemani ametoa  maagizo  kwa viongozi wa Tanesco katika ngazi ya Mkoa na Wilaya kuhakikisha umeme huo unawaka kwa wakati.

Naye Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Abdallah Ulega amesema  wananchi katika vijiji ambavyo vilitakiwa kupata umeme walikata minazi na miembe yao ili kupisha miundo mbinu ya umeme lakini ni zaidi ya miaka mitano tangu miundombinu ya umeme iwekwe na hakuna umeme.

Aidha Ulega amemshukuru Waziri Kalemani kwa ziara yake jimboni hapo kwani anaamini italeta mabadiliko na amewataka watendaji waliopewa maagizo na Waziri wayafanyie kazi mara moja.
 Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani(katikati)kwa kushiriki na viogizo mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme katika kijiji cha Mkokozi Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (alienyosha mkono) akizungumza na wanachi wa kata ya Kisiju wilaya ya Mkuranga  ambapo amewaagiza  watendaji wa Tanesco siku  14  wahakikishe umeme umewaka (Picha Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa  kijiji cha Kisiju ambapo amemshukuru Waziri Kalemani kwa ziara yake jimboni.
 Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga  wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...