Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Njombe na Halmashauri yake pamoja na uongozi wa kiwanja cha ndege cha mkoa huo kuona namna ya kuziondoa nyumba zote zilizopo mita 500 kutoka katika kiwanja hicho ili kupisha ujenzi unaotarajiwa kufanyika katika kiwanja hicho hivi karibuni. 

Waziri Mhandisi Kamwelwe ametoa wito agizo hilo mkoani humo mara baada ya kutembelea kiwanja hicho na kujionea nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya kiwanja hicho. Amesema kuwa ujenzi wa makazi hayo umesababishwa na Halmashauri kupima viwanja mpaka kwenye maeneo ya kiwanja hicho hivyo ni lazima waangalie namna sahihi ya kuwahamisha wakazi hao kwa kuwalipa fidia kwa wale wnaaostahili. 

“Kiwanja hiki kipo eneo zuri la tambarare, lakini tumeona wenyewe wananchi wamejenga hadi magorofa katika maeneo karibu ya kiwanja hivyo ni lazima waondolewe ili kupisha ukarabati na watakaoonekana wanahaki ya kufidiwa wafidiwe,” amesema Waziri Mhandisi Kamwelwe. 

Aidha, Mhandisi Kamwelwe amefafanua kuwa eneo hilo ambalo limejengwa ndio linalotumiwa na ndege kupaa, hivyo kama itashindwa kupaa au kutua inaweza kutua juu ya paa la nyumba ya wakazi hao na kusababisha maafa. Ameongeza kuwa Serikali ina mpango wa kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa mkoani humo hivyo ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili
kuhakikisha ujenzi huo unaanza. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege Njombe Bi. Hana Kibopile (wa pili kulia), wakati akikagua Kiwanja hicho, mkoani Njombe. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka, akimuonesha maeneo yaliyovamiwa na wananchi katika Kiwanja cha Ndege cha Njombe Waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati alipokuwa akikagua kiwanja hicho.

Muonekano wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Njombe. Kiwanja hicho ni miongoni mwa viwanja 11 vilivyopo katika mpango wa kujengwa na Serikali ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoani humo. 
Muonekano wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania. 



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...